Kimya tafadhali ! Jinsi kupunguza kelele kunavyoongeza nguvu ya ubongo na ubunifu

Indian arch silhouette in old temple at dramatic orange sunset sky background.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sikiliza... sauti ya ukimya

Tunazungukwa na sauti na makelele, lakini nini hutokea pale tunapotawaliwa na ukimya?

Kelele za magari, ving'ora, sauti kubwa, milio ya simu na kengele za taarifa kwenye mitandao ya kijamii, muziki na kadhalika, na kadhalia - ndiyo inachosha...lakini bado wengi wanaamini ukimya ni dalili ya upweke.

"Tunaishi kwenye zama za makelele. Ukimya ni kama vile umeshatokomea," anasema Mwanafalsafa na mtembezi Erling Kagge.

Anajua akisemacho: ameshafika sehemu ambazo zimetawaliwa na ukimya ulio mkuu. Matembezi yake yamemfanya kuwa binadamu wa kwanza kufika kwenye 'mihimili mikuu mitatu' ya dunia. Mhimili wa kusini (pembe ya kusini zaid ya dunia) mhimili wa Kaskazini (pembe ya kaskazini zaidi ya dunia) na kilele cha mlima Everest, ambao ndio mlima mrefu zaidi duniani.

Hivyo, kwa nini tunitaji ukimya? Na tuliupoteza vipi?

Na la muhimu zaidi, tutaurudisha vipi ukimya?

Ukimya unaturuhusu tuhisi uwepo wetu

Chanzo cha picha, Getty Images

"Antarctica ndiyo sehemu ya ukimya zaidi ambayo nimeshawahi fika" anasema Erling, "Ilinifanya kuhisi uwepo wangu katika dunia. Hakukuwa na ukelele wowote, ilikuwa ni mimi na mawazo yangu tu."

Si wote ambao tunaweza fika kule ambapo mtembezi huyo amefika ili kuona nguvu ya ukimya. Lakini tunaweza kupata maeneo tulivu katika mazingira yatuzungukayo.

Iwe chumbani, kwenye kona ya bustani, ama msalani twaweza pata ukimya utakaoshusha mzigo wa shughuli zetu ngumu nza za kuchosha tuzifanyazo kila siku.

Erling anaamini kuwa, wote tunaweza kupata "ukimya wa ndani" na kushauri "kusimama bafuni .... kuota kijinga cha kuni, kuogelea kwenye mto ama bwawa msituni, ama kutembea kwenye eneo tulivu, vyote vinaweza kufanya mtu kuingia kwenye dimbwi la utulivu."

Ukimya unatupa nafasi ya kufikiri

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukimya ni "ufunguo wa njia mpya za kufikiria," anasem Erling, na sayansi inathibitisha nadharia hiyo.

Hata bila ya kuchochewa na sauti, bongo la mwanadamu bado lingali fanya kazi na kuchangamka.

Utafiti mmoja wa mwaka 2001 uliofanywa na wanasayansi wa mfumo wa fahamu kutoka Chuo Kikuu cha Washington Marekani ulibaini kuwa kupitia mfumo maalumu, ubongo uliopumzika bado unakuwa kazini na mara kwa mara huchambua taarifa.

Tafiti zilizoendelea zilionesha kuwa mfumo huo husaidia binadamu kujitathmini.

Ukimya na mapumziko ndiyo ufunguo wa namna bora ya kufikiri kwa ubunifu kwa nmna bora kabisa.

Ukimya ni nyenzo ya nguvu kwenye mazungumzo

Chanzo cha picha, Getty Images

"Ukimyani moja ya sanaa kubwa ya mazungumzo," kama alivyopata kusema mshairi wa Kirumi aitwae Cicero.

Katika mazungumzo au mabishano, ni rahisi kusahau nguvu ya ukimya - lakini kukaa kimya kunaweza kukawa nyenzo kuu, ni maamuzi ambayo tunayo.

Ukimya unakupa nafasi ya kujipanga nini cha kusema baada ya mpinzani wako.

Lakini pia ni hali inayoonesha namna gani unajiamini katika hoja yako. "Hakuna kinachoongeza nguvu ya utawala kama ukimya," alisema Leonardo da Vinci.

Ukimya unaweza kusaidia ubongo kukua

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwaka 2013, mwana bailojia Imke Kirste alikuwa akifanya majaribio juu ya athari za sauti kwenye ubongo wa panya.

Matokeo yalikuwa yakushangaza, sauti hazina madhara ya kudumu. Lakini saa mbili za utulivu kwa siku zinachagiza pakubwa ukuaji wa seli za ubongo zinazojenga kumbukumbu.

Endapo uhusiano kama huu utabainika kwa binaadamu basi wanasansi watapigia chapuo ukimya kutumika kama sehemu ya matibabu kwa wanaokumbwa na msongo wa mawazo.

Dawa ya mitandao ya kijamii

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kusubiria kelele kutoka kwenye kioo cha simu yako ni aina ya uraibu," ameonya Erling.

"Kadri tunavyosubiria, ndivyo kadri tunavyokuwa waraibu...tunaangalia simu muda wote kama jeshi la kibaka mmoja ili kusuuza matamanio ya nafsi."

Lakini kusbiria starehe ama kuukongga moyo kwa njia ya makelele kuna athari kubwa. Simu na mitandao ya kijamii hufanya watu kujenga ukuta wa mawasiliano na mapenzi na familia ama watu wao wa karibu.

Japo yawezekana kuwa kazi ngumu mwanzoni, lakini ni vyema kwa watu kujaribu kuzima mitandao ya kijamii walau kwa saa chache kwa siku.

Ukimya husaidia kuondosha msongo wa mawazo

Chanzo cha picha, Getty Images

Florence Nightingale ameandika kuwa: "Kelele zisizo za lazima ni namna mbaya zaidi ya ukatili ambayo anaweza kufanyiwa mgonjwa ama mtu ambaye ni mzia wa afya."

Nesi huyo maarufu wa karne iliyopita pia amesema sauti zisizo za lazima zinaweza kuchochea taharuki, uchovu, msongo wa mawazo na kukosa usingizi kwa wagonjwa.

Tafiti za kisayansi za miaka ya hivi karibuni zinaunga mkono mawazo yake.

Kuna uhusiano wa dhahiri kati ya kelele kama za uwanja wa ndege ama barabarani na shinikizo kali la damu.

Kelele pia huchochea viwango vikubwa vya msongo wa mawazo.

Kwa upande wa pili, ukimya, hauna athari kama hizo maana husaidia mwili na akili kupata utulivu.

Tafiti iliyochapishwa kwenye jarida la Moyo umeonesha kuwa dakika mbili za ukimya zinaweza kukutuliza kuliko kusikiliza muziki wa "kutuliza".