Uchaguzi Nigeria 2019: Atiku Abubakar dhidi ya Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (kushoto) na mpinzani wake Atiku Abubakar wakipiga kura

Chanzo cha picha, REUTERS/AFP

Maelezo ya picha,

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (kushoto) na mpinzani wake Atiku Abubakar wakipiga kura

Mamilioni ya watu nchini Nigeria hatimaye leo wameshiriki uchaguzi mkuu baada ya shughuli hiyo kuahirishwa ghafla wiki moja iliyopita.

Kufikia sasa shughuli ya kuhesabu kura imeanza umeanza.

Wagombea wawili wakuu ni rais Muhammadu Buhari, 76, na naibu wa rais wa zamani Atiku Abubakar, 72.

Bw. Buhari anasema amejenga msingi thabiti wa ustawi wa jamii lakini mpinzani wake anadai miundo mbinu ya utawala haifanyi kazi Nigeria.

Yeyote atakayeshindi uchaguzi huu anakabiliwa na kibarua cha kushughulikia masuala ya uhaba wa umeme, ufisadi, tishio la usalama na mdororo wa uchumi.

Haijabinika matokeo ya uchaguzi yatatolewa lini - Huenda ikawa Jumatatu, Jumanne, ama baadae.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Karatasi ya kupigia kura ya wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2019

Kwanini Uchaguzi ulicheleweshwa?

Uchaguzi wa awali ulikuwa umepangiwa kufanyika Jumamosi ya Februari 16 lakini Tume huru ya uchaguzi (Inec) ikatangaza kuahirishwa kwa shughuli hiyo saa tano kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.

Tume hiyo imetoa sababu kadhaa ya kuchelewesha uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na jaribio la kuhujumu shughuli hiyo, changamoto za kiufundi na hali mbaya ya hewa.

Inec hata hivyo imethibitisha kuwa mara hii iko tayari kuendesha uchaguzi huo.

Mchakato wa uchaguzi huishia vipi?

Mgombea atakayepata kura nyingi ndiye atakayetangazwa mshindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi ili mradi amejizolea angalau 25% ya kura katika thuluthi mbili ya majimbo 36 nchini Nigeria.

Kuna wagombea jumla ya wagombea 73 wa uraisi, lakini kampeini zilizoangaziwa zaidi ni ya kati ya wababe wawili wa kisiasa na washirika wao waliyokuwa wakifanya kazi nyuma ya pazia.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Muhammadu Buhari amepiga kura katika kituo cha Daura, Jimbola Katsina

Chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kimeahidi kuipeleka nchi katika "hatua nyingine", akisema kuwa miaka minne ya kwanza ya utawala wa Buhari ulikuwa wa "kuunda mfumo wa kazi" japo matokeo ya kazi hiyo huenda hayakuonekana.

Bwana Abubakar na chama chake cha People's Democratic Party wameahidi "kuiwezesha Nigeria kufanya kazi tena", wakiongeza kuwa rais amewapotezea miaka minne.

Wote wawili wanatokea eneo la Kaskazini lililo na waumini wengi wa dini ya kiislamu.

Japo wako katika miaka yao ya 70 zaidi ya nusu ya wanigeria milioni 84 waliyojiandikisha kupiga kura wako chi ya miaka 35.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Masuala makuu ni yapi?

Nigeria ni mzalishaji mkuu wa mafuta barani Afrika lakini ufisadi na ukosefu wa kuwekeza fedha zinazotokana na sekta ya mafuta umerudisha nyuma maendeleo katika taifa hilo la Afrika magharibi.

Ilikumbwa mzozo mkubwa wa kiuchumi mwaka 2016 na imekuwa ikijijikakamua kujinasua katka mzozo huo japo hakuna nafasi ya ajira iliyobuniwa kukabiliana na idadi kubwa ya vijana ambao hawana kazi.

Kwasas karibu robo ya watu waliyofikisha umri ya kufanya kazi hawana ajira.

Takwimu za uchaguzi

  • Watu milioni 84 wamejisajili kupiga kura
  • 51% ya waliyojisajili kupiga kura wako chini ya miaka 35
  • Kuna jumla ya wagombea uraisi 73
  • Vituo vya kupiga ni 120,000

Rais Buhari amejaribu kudhibiti shughuli za wanamgambo wa kundi la kiislam katika maeneo ya kaskazini mashariki,lakini wanamgambo hao wameendelea kuhangaisha utawala wake.

Pia kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulizi katika maeneo ya kati ya nchi hiyo ambako jamii ya wafugaji imekuwa ikizozana na wakulima.

Hadi mwaka 1999 Nigeria imekuwa ikiongozwa na utawala mfupi wa kiraia ama wa kijeshi.

Mwaka huu unaadhimisha miaka 20 ya kurejea kwa utawala wa kidemokrasia .

Bwana Buhari alichaguliwa mwaka 2015 - na kuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kumshinda rais aliyekuwa madarakani.