R Kelly: Mwanamuziki maarufu wa Marekani ameshitakiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono

R Kelly alivuma kwa vibao vyake Ignition na I Believe I Can Fly

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

R Kelly alivuma kwa vibao vyake Ignition na I Believe I Can Fly

R Kelly ameshitakiwa na makosa 10 ya dhulma za kingono tisa kati ya hizo ikihusisha watoto wadogo.

Nyota huyo wa muziki wa R&B ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, amekabiliwa na madai ya dhulma za kingono dhidi ya wanawake na watoto kwa miongo kadhaa.

Kelly hajawahi kushitakiwa na amekuwa akikanusha madai hayo kwa muda mrefu.

Mahakama ilichukua hatua hiyo baada ya ukanda wa video kuonesha tukio lililotokea 1998 na kuhusisha wasichana 4.

R Kelly mwenye umri wa miaka 52 alijisalimisha kwa polisi mjini Chicago baada ya kibali cha kukamatwa kwake kutolewa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kelly alijisalimisha kwa polisi usiku wa Ijumaa

Wakili wake ameelezea kuwa "amegutushwa sana na uamuzi huo".

Steve Greenberg aliliambia gazeti la Associated Press kuwa mteja wake"ameathiriwa vibaya" na mashtaka hayo na kusisitiza kuwa hana makosa.

Madai dhidi yake ni yapi?

Mahakama ya Chicago siku ya Ijuma ilitoa amri ya kukamatwa kwa mwanamuziki wa R&B R.Kelly kufuatia ushahidi mpya kuhusiana na madai aliwadhulumu kimapenzi watoto kati ya miaka 13-17.

Mashitaka hayo yanakuja wiki kadhaa baada ya makalaya hivi karibuni inayoitwa , 'Surviving R Kelly', ambayo ilikuwa inaoneshwa katika chaneli moja ya televisheni inayoitwa lifetime,kuangazi namna ambavyo amefafanua madai yake dhidi ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kelly aliwahi kuondolewa mashitaka ya kuhusika na filamu za utupu zinazohusisha mwaka 2008

Hata hivyo wakili wa Kelly amesitisha makala hiyo isiendelee kutumika.

Kiongozi wa mashtaka wa Kim Foxxamesema mwanamuziki huyo huenda akfungwa miaka saba kwa kila kosa akipatikana na hatia .

Greenberg,wakili wake, amelimbia shirika la habari la AP kuwa aliomba kufanya kikao na viongozi wa mashtaka kuelezea kwanini "mashitaka haya hayana msingi wowote" lakini walikataabut said they refused.

Mashitaka haya yalifikiwa vipi?

Mwanasheria mkuu wa Cook County Kim Foxx alitoa wito kwa wanawake kutoa ushahidi baada ya makala ya makala ya 'Surviving R Kelly' kupeperushwa hewani.

Wakili Michael Avenatti amesema kuwa anawawakilisha watu sita, wawili kati yao ni waathiriwa waaliyodai kunyanyaswa na Kelly katika makala hiyo.

''Angalau mmoja wao amejumuishwa katika mashitaka yaliyothibitishwa na mahakama siku ya Ijumaa'', alisema.

Bwana Avenatti alilijitokeza wiki iliyopita na kuwakabidhi waendesha mashitaka kanda ya video inayomuonesha Kelly akifanya ngono na msichana mdogo.

Wakili huyo alisema kuwa kanda hiyo inayokadiriwa kuwa dakika 40 ilinaswa mwaka 1999 na inamuonesha mwanamuziki huyo akifanya mapenzi na mttoto wa miaka 14.

Alidai kuwa Kelly na msichana huyo walirudia "neno miaka 14" mara kadhaa katika video hiyo.

Kelly aliwahi kuondolewa mashitaka ya kuhusika na filamu za utupu zinazohusisha mwaka 2008

Mwaka 2017, R. Kelly alikana madai kwamba anawazuia wanawake kadhaa katika dhehebu lake analotumia kuwanyanyasa.

Wakili wa mwanamuziki huyo alisema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa wale wanaomtuhumu anawakabili kisheria ili kusafisha jina lake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

kumekuwa na miito ya kususia muziki wa R Kelly katika mitandao ya kijamii kupitia hashtag #MuteRKelly

Kutokea wakati huo wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwa kuwaomba watu kususia muziki wake kupitia hashtag #MuteRKelly.