Mwanaume mmoja aandika waraka akitahadharisha watu wasivute sigara kabla ya kifo chake

Geoff Turner

Chanzo cha picha, Sarah Huiest

Maelezo ya picha,

Geoff Turner

Mwanaume mmoja 66 jimboni New York nchini Marekani aliandika historia ya maisha yake akitahadharisha watu kutovuta sigara.

Geoffrey Turner alipoteza maisha tarehe 13 mwezi Februari baada ya kuugua saratani ya mapafu kutokana na uvutaji sigara kwa miongo kadhaa.

''Nilikua mpumbavu, nilikua nafanya makosa ya kijinga, siku baada ya siku,'' Bwana Turner aliandika. ''kama wewe ni mvutaji-acha sasa- .''

Binti yake, Sarah, aliiambia BBC kuwa anajivunia kitendo cha baba yake kuandika waraka huo.

''Nilikua mvutaji na ingawa nilijua hatimaye nitakufa, nilichagua kutojali ukweli kuhusu tabia yangu,''

Alibainika kuwa na saratani mwezi Novemba mwaka jana,akiwa na saratani iliyofikia hatua ya nne, Daktari wake alisema ni matokeo ya uvutaji wa miaka mingi.

''Maumivu na mahangaiko niliyoisababishia familia yangu kwa sababu ya 'kujifurahisha', furaha ambayo haikunifikisha popote zaidi ya kupoteza pesa, kunitenga na familia yangu, na hatimaye kuuharibu mwili wangu.''

Niliishi maisha safi, lakini kuna matukio mengi ambayo sitaweza kushirikisha ninaowapenda,''aliandika.Funzo la hadithi hii-usiwe mjinga.

''Kumbuka, maisha ni mazuri-usiyapoteze kwa moshi wa sigara.''

Sarah Huiest ameiambia BBC kuwa alishtuka Baba yake alipomuonyesha waraka wake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wataalamu wanasema wavutaji wa sigara wako hatarini kupata saratani

Waraka huo umepokelewa vizuri. ''Marafiki na wale nisiowafahamu waliniambia namna ambavyo wangependa maneno ya waraka kama huo wangeyapata kutoka kwa wapendwa wao.'' alieleza Bibi Huiest

Ameiambia BBC kuwa Bibi yake kwa amara ya kwanza alifuma Bwana Turner akivuta sigara, yeye akiwa na miaka miwili, na baba yake anakumbuka alianza na tabia ya uvutaji akiwa na miaka minne.

Awali bwana Turner alisitisha kuvuta sigara baada ya kumuoa Mama Sarah, lakini aliporejea tena kwenye uvutaji katikati ya miaka ya 90 akiwa kwenye safari ya kibiashara jijini London, na hakuacha tena mpaka alipogundulika kuathiriwa na saratani mwaka jana.

Lakini hakuwahi kuvuta mbele ya watoto wake, Binti yake alieleza.

''Wakati wote tulipokuwa tukikua miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, alikua akizungumza dhidi ya uvutaji akitutaka tuepuke.''

Vituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani vinasema uvutaji sigara ni sababu kuu ya maradhi yanayoweza kuzuilika na sababu ya vifo nchin humo, watu takribani nusu milioni wakipoteza maisha kutokana na uvutaji kila mwaka.