Oscars 2019: Washindi wa Black Panther waweka historia

Ruth Carter

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Ruth Carter was responsible for creating the outfits in Black Panther

Presentational white space

Washirika wawili katika filamu ya Black Panther wameweka historia katika tuzo ya Oscar kwa kuibuka washindi wa kwanza weusi katika vitengo walivyoshinda.

Ruth Carter alijizolea tuzo ya mbunifu bora wa mavazi na Hannah Beachler alishinda tuzo ya ubunifu wa filamu kwa pamoja na mshindi mwingine Jay Hart.

"Lilitarajiwa kwa muda mrefu," Carter amesema katika hotuba yake. "Huenda Marvel imeunda shujaa wa kwanza mtu mweusi lakini kwa kutumia mavazi ya ubunifu tulimgeuza kuwa mfalme wa Afrika."

Mshindi mwenza wa Oscar Halle Berry ni mojawapo ya waliotangualia kumpa hongera.

Filamu nyingine alizobuni Carter ni pamoja na Amistad, Malcolm X na Selma.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Jay Hart was responsible for set decoration and Hannah Beachler did production design

Wakati huo huo , Beachler - ambaye amewahi kushughulika katika filamu ya Moonlight, Creed n akibao cha Beyonce Lemonade - alitoa heshima kwa mkurugenzi wa filamu ya Black Panther Ryan Coogler.

"Nasimama thabiti kuliko nilivyokuwa jana," amewaambia watu waliokusanyika katika tuzo hiyo.

"Nasimama hapa kwasababu ya mwanamume aliyenipa mtazamo tofuati wa maisha, aliyenipa mahala salama, aliye na subira na aliye na utu na undugu.

"Asante Ryan nakupenda."