Uwindaji haramu ya ndovu nchini Botswana 'si uongo'

Tembo nchini Botswana

Chanzo cha picha, AFP

Moja ya hifadhi ya tembo barani Afrika inakabiliwa na "tatizo kubwa la uwindaji haramu wa pembe za ndovu '', kwa mujibu wamatokeo ya mwisho ya uchunguzi wa wanyamapori nchini Botwana ulioangaliwa na BBC.

Shirika la wanyamapori la Elephants Without Borders, lililofanya utafiti wa miaka minne kwa ushirikiano na serikali, linasema kuna ongezeko mara sitala kiwango kipya ''mpya au cha "hivi karibuni " cha masalia ya mizoga ya tembo kaskazini mwa Botwanaambayo ni ''ishara wazi" ya uwindaji haramu wa ndovu.

Mike Chase, mwanasayansi aliyefanya utafiti huo, aliibua mjadala mkali nchini humo alipotoa shutuma zake wazi wakati uchunguzi wake haujakamilika mwezi Agosti mwaka jana, akisema kuna wizi wa pembe za ndovu na kudai maafisa wanampuuza.

Aliiambia BBC wakati huo kwamba alipokuwa akisafiri kwa ndege kaskazini mwa Botswana, aligundua kuwa tembo 87waliuawa hivi karibuni katika eneo moja - na sasa idadi imeongezeka hadi 88 - na kwa ujumla tembo waliouawa ni 128.

Serikali imeitaja idadi kiyo kuwa ni " uongo na ya kupotosha" na ikakosoa kile ilichokotaja kuwa ni "ripoti za vyombo vya habari zisizokuwa na mashiko zenye uchochezi ".

Alipokea vitisho vya kuuawa na tangu wakati huo serikali ilimpokonya moja ya vibali vyake viwili vya utafiti.

Maeneo yaliyokumbwa na biashara haramu ya ndovu

Aliyekuwa rais wakati huo Mokgweetsi Masisi alielezea madai kama "taarifa za uongo kuwahi kutolewa katika karne ya 21 " na akakanusha kuwa kumekuwepo na ongezeko labiashara ya ndovu nchini mwake.

Lakini ripoti ya mwisho ilibainisha maeneo manne ya biashara haramu ya ndovu , ikitoa ushahidi wa picha zilizochukuliwa na watafiti waliozulu eneo maeneo hayo na kuthibitishwa na wataalamu tisa wa kimataifa wa masuala ya ndovu.

"Jibu kutoka kwa watu tofauti lilikuwa ni kujaribu kukanusha au kuficha ukweli na kunipachika jina la usaliti na muongo- bila hata kuthibitisha ushahidi wa yale tuliyo yashuhudia ," alisema Bwana Chase.

Maelezo ya picha,

Mike Chase alisema kwa kuwa alishuhudia ongezeko la mizoga ya tembo kaskazini mwa Botswana

Serikali haikujibu ombi la BBC la kufanya mahojiano juu ya ripoti ya mwisho , lakini ilitoa taarifa iliyokosoa njia zilizotumiwa katika kufanya utafiti.

Taarifa iliyotolewa Thato Raphaka, Katibu wa kudumu katika wizara ya mazingira , hifadhi ya mali asili na utalii, ilisema ''inasikitisha" kwamba ripoti ilionyesha "idadi ya kushangaza ya picha za mizoga ya ndovu'' .

Ilikosoa baadhi ya maelezo ya kisayansi katika ripoti na ikaomba data za awali ziwasilishwe katika kundi la wataalam wa ndovu la International Union for Conservation of Nature kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi huru.

Otisitwe Tiroyamodimo, mkurugenzi wa idara ya wanyamapori na mbuga za wanyama , alisema serikali inakubali kuwa tatizo la uwindaji haramu lipo.

"Hakuna yeyote anayekanusha kwamba tembo wanauawa nchini Botswana," lakini wale walioripotiwa na Bwana Chase walikufa ''kutokana na vifo vya kawaida na vya ulipizaji kisasi''

"Tulikwenda pale na hatukupata mizoga 87 ," alisema Bwana Tiroyamodimo.

Kutoweka kwa pembe za ndovu

Maafisa waliosafiri na Bwana Chase hata hivyo wanakiri kuwa wlaitumia siku mbili tu kujaribu kuthibitisha kuthibitisha mizoga iliyoonekana kwa miezi miwili.

BBC ilipewa jukumu la kuratibu moja ya maeneo manne yaliyotambuliwa kama '' vitovu vya mauaji ya ndovu'' na timu ya watafiti na tulitembelea maeneo 67 ya mizoga.

Botswana ina jumla ya tembo 130,000 - ikiwa ni sawa na theluthi mbili ya idadi nzima ya ndovu wanaopatikana barani Afrika - kwa hiyo si jambo la kushangaza kuwa ni mlengwa mkuu wa wafanyabiashara haramu wa ndovu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ndovu

Mzozo wa muda mrefu wa kisiasa

Rais Masisi alikuwa makamu wa rais hadi Aprili 2018, wakati rais aliyekuwa rais Ian Khama alipo kabidhi mamlaka kwa naibu wake.

tangu wakati huo viongozi hao hawapatani.

Maelezo ya video,

Fahamu manufaa ya ndoto mbaya ulio iota

Rais mpya ana maono mapya juu ya masuala kadhaa, mkiwemo uhifadhi wa maliasili na ameondoa baadhi ya sera za awali.

Uwindaji ulipigwa marufuku chini ya rais Khama na Botswana ilijulikana kama nchi isiyovumilia kabisa uwindaji haramu

Iliripotiwa kwamba mwaka 2015 pekee Wanamibia 30 , Wazimbabwe 22 na idadi ya Wazambia isiyofahamika walipigwa risasi baada ya kushukiwa kwa uwindaji haramu.

Maelezo ya picha,

Faru kumi na watatu pia waliuawa na wawindaji mwaka jana

David Kays, anayemiliki kampuni ya utalii wa wanyamapori ya Ngamiland Adventure Safaris katika eneo la Okavango Delta, amesema kuwa muda umefika wa kukubali kwamba kuna tatizo la uwindaji haramu na kushirikiana kukabiliana nalo.

" Ninadhani serikali imekuwa ikificha kwa muda na sasa kwasababu suala hili limewekwa wazi tmetambua ni kwa namna gani tatizo hili ni kubwa na wawindani haramu wamebainika kuliko ilivyo tarajiwa.

Maelezo ya picha,

Kim Nixon kutoka kampuni ya Wilderness Safaris anasema matukio yote ya uwindaji yanaripotiwa

Wilderness Safaris hufanyia kazi zake katika hoteli ya kifahari ya luxury lodges katika moja ya maeneo ambapo baadhi ya mizoga 88 ya ndovu ilipatikana.

Mkurugenzi wake mkuu Kim Nixon alipinga taarifa zozote kwamba hakuna tatizo la uwindaji haramu.

"Wakati wowote kulipotokea tukio la uwindaji haramu kwenye eneo letu liliripotiwa kama tukio la uhalifu ," alisema.

Bwana Chase anasema " usimlaumu aliyetumwa" akiongeza kusema kuwa : Ninadhani inahitaji wadau wote kushirikiana na kwa pamoja -serikali, watu binafsi na sekta binafsi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ."

Botswana bado ni mahali salama duniani kwa ndovu na faru duniani, lakini kutokana na kuendelea kuwepo kwa haja kubwa ya pembe za ndovu barani Asia, ni dhahiri kwamba sasa inaangaliwa zaidi na wawindaji haramu.