Waliomzaba kofi polisi mwanamke wa usalama barabarani Uganda nguvuni

Rebecca Kadaga
Maelezo ya picha,

Spika wa bunge la Uganda Rebecca kadaga

Spika wa bunge la Uganda ameshtumu vikali vitendo vya majeshi walinzi pamoja na meja jenerali mmoja mstaafu cha kumhujumu askari polisi mwanamke wa usalama barabarani mwishoni mwa wiki.

Picha za kuhujumiwa kwa mwanamke huyo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeibua hasira kubwa miongoni mwa wananchi, huku taasisi za jeshi na polisi zikimkosoa Jenerali huyo ambaye pia ni balozi wa Uganda nchini Burundi.

Mvutano kati ya walinzi wa Meja Generali Matia Kyaligonza na polisi mwanamke ambaye ni polisi wa usalama barabara aliyewazuia kukiuka sheria za barabarani ulishuhudiwa na umma mtaa wa Seeta.

Askari huyo kwa jina Esther Namaganda alionekana kwende ukanda mfupi wa video uliochukuliwa na mtu aliyeshuhudia tukio hilo.

Mmoja wa askari anaonekana akiuvuta mkono wa Sajenti Esther Namaganda ambaye anajaribu kukabiliana naye. Meja Generali Matayo Kyaligonza, ambaye anaonekana akiwa amevalia shati jeupe , alikuwa akizunguka eneo la tukio hilo akiwa ameshikilia bakora. haonekani akijaribu kuwazuwia walinzi wake kumvuta afisa wa usalama bara baraniau kuwashambulia watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo.

Badala yake kwenye ukanda huo wa video, Jenerali Kyaligonza alionekana akijaribu pia kumvuta Sajenti Namaganda.

Kulingana na Sajenti, Generali pia alimzaba kofi usoni , ingawa picha zilizosambazwa za tukio hilo hazimuonyeshi akifanya hivyo.

Msemaji wa jeshi la Brigadia Uganda Genera Richard Karemeire ameomba radhi kwa shambulio dhidi ya Esther Sajenti Namaganda ''Tunaomba msamaha kwa askali polisi Sgt., hata hivyo habari njema ni kwamba sisi kama jeshi la Uganda (UPDF) tumechukua hatua za haraka kwa hao askari wawili wamekamatwa na upelelezi unaendelea kwa pamoja na polisi na baada ya hapo hatua kali zitachuliwa dhidi yao'', amesema.

Spika wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga amelaani vikali vikali kitendo hicho wakati alipokutana na wanaharakati wa haki za wanawake waliowasilisha malalamiko kwake. ''Tabia hii ya kumshambulia mtu ambaye anafanya kazi aliyopewa na serikali haikubaliki haikubaliki miongono mwa viongozi na mtu mwingine yeyote haikubaliki, nafurahi kwamba wahusika wamekamatwa na ningemtaka mkuu wa jeshi la polisi kumpandisha cheo mwanamke huyo''. Alisisitiza Spika kadaga.

Bi Angela Asiimwe msemaji wa msemaji wa kundi la wanaharakati wa haki za wanawake nchini Uganda.

alisema ''Ulikua ni ukiukaji mkubwa wa haki zetu wanawake na waganda kwa ujumla, nafurahi kwamba baadhi ya waliompiga Sajenti Namaganda wamekamatwa''

Si mara ya kwanza kwa Jenerali Kyaligonza kulaumiwa kwa tukio kama hili. Mwaka 1989 alishushwa cheo kwa kumzaba kofi afisa wa polisi.

Mwaka 2001 alidaiwa kumpiga mwandishi wa habari na mwezi Mei mwaka jana alishutumiwa kumpiga jirani yake.

Akiwa ni afisa wa ngazi ya juu jeshini aliyemsaidia rais Yoweri Museveni Kuingia madarakani mwaka 1986, huenda wengi wakasubiri kuona ikiwa matendo yake yatachunguzwa au la.