Maandamano Sudan: Kwanini hali ya hatari aliyoidhinisha rais Omar al Bashir haifanyi kazi?

Waandalizi wa maandamano wameapa kuendelea na mpango huo kila siku

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Waandalizi wa maandamano wameapa kuendelea na mpango huo kila siku

Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir alitangaza hali ya hatari nchini humo Ijumaa iliyopita katika jaribio la kuzima maandamano ya wiki 10 ambayo yametishiautawala wake wa miaka 30.

Waandamanaji hatahivyo wamekaidi amri hiyo licha ya mkusanyiko wa watuk upigwa marufuku kwa mujibu ya wa shirika la habari la Reuters.

Tangazo la bwana Bashir lilitarajiwa na waandamanaji ambao walimiminika katika barabra za mji mbali mbali hata kabla akamilishe hotuba yake kwa taifa siku ya Ijumaa.

Tangu wakati huo maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana katika mji mkuu wa Khartoum na Omdurman.

Chama cha Umma National party, waandalizi wa maandamano hayo, chama cha wafanyikazi nchini Sudan, wote wamepinga tangazo la rais Bashir.

Wanasema wataendelea na maandamano hayo hadi pale rais atakapong'atuka madarakani.

Maelezo ya video,

Je ni nini kinafanyika ndain ya vizuizi vya siri Sudan?

Vikosi vya usalama vimeanza tena kutumia risasi dhidi ya waandamanaji, kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka mrengo wa upinzani.

Vinadai kuwa watu watatu walipigwa risasi siku ya Jumapili.

Msako mkali umefanywa kuwasaka wanaharakati wa upinzani katika eneo la Burri nje kidogo ya Khartoum.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kumekuwa na maandamano kote Sudan kumshinikiza Rais Bashir kuondoka madarakani

Katika hotuba yake kwa taifa bwana Bashir ameliomba bunge kuahirisha mchakato wa marekebisho ya katiba ambao ungemruhusu kugombea muhula mwingine madarakani.

Bashir pia kufutilia mbali utawala wa majimbo na uongozi wake..

Rais alisema nini?

Kumekuwa na fununu kuwa rais Bashir atatangaza kuachia madaraka lakini hakufanya hivyo

Kujiuzulu kwake kama rais ni moja ya matakwa ya kukomeshwa kwa maandamano dhidi ya serikali ambayo yalianza katikati ya mwezi Desemba.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kumekuwa na fununu kuwa rais Bashir atatangaza kuachia madaraka

Baadhi ya waangalizi wa siasa nchini Sudan wamehusisha hali inayoshuhudiwa nchini humo na tofauti iliyoibuka kati ya bwana Bashir na "godfather", wake katika kundi maarufu la kiislam,marehemu Hassan al-Turabi mwaka 1999.

Wakati huo, Bwana Bashir alivunja bunge na utawala wa katiba katika hatua ambayo ilisababisha mgawanyiko mkubwa katika wa vyama vikuu vya kisiasa.

Siku ya Jumatatu taarifa ya vyombo vya habari vya Sudan iliashiria kuwa viongozi wa ngazi ya juu ya wa NCP wanatafakari uwezekano wa kumchagua kiongozi mkuu wa chama.

Mmoja wa viongozi hao stalwart, Amin Hassan Omar, ameliambia gazeti la al-Intibaha kuwa rais amejilimbikizia madaraka yote ili chama kisionekane kinatawala nchi.

Hatahivyo haijabainika ikiwa bwana Bashir atajitenga kabisa na chama cha NCP kama ilivyofanyika mwaka 1999, au ni mkakati wa kisiasa unaolenga kuwachanganya mahasimu wao.