Hadhara Charles Mnjeja: Mwanadada aliyemvutia Trump kwa ustadi wake wa kupepeta mpira

Hadhara Charles Mnjeja: Mwanadada aliyemvutia Trump kwa ustadi wake wa kupepeta mpira

Video fupi inayomuonesha mwanadada Hadhara Charles Mnjeja kutoka Tanzania, akipepeta mpira kwa ustadi imepata umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Rais wa Marekani Donald Trump alitambua kazi ya Hadhara na kuandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa ni kipaji kinacho stahili kukuzwa.

Mchezaji huyo wa miaka 29 yuko nchini Malawi hadi mwezi Machi ambako anajipatia riziki kupitia onyesho lake kupepeta mpira mitaani.

Analipisha dola tano kwa dakika mbili. Je anasemaje baada ya kutambuliwa na Trump?

"Nashukuru kuwa rais Trump anajua jina langu. Hatahivyo namuomba anisaidie kukuza kipaji changu kiwe baishara imara."