Bin Laden: Marekani yatangaza kitita kwa taarifa kumhusu mwanawe Osama, Hamza

State Department's Wanted poster Haki miliki ya picha Rewards for Justice/State department
Image caption Hamza Bin Laden's whereabouts are not known

Marekani imetangaza $ milioni 1 kwa taarifa kuhusu mwanawe wa kiume kiongozi wa kundi la al-Qaeda - Osama Bin Laden, Hamza.

Hamza Bin Laden anainukia kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu imesema wizara ya mambo ya nje.

Katika miaka ya hivi karibuni, ametoa kanda za video na sauti ambapo anatoa wito kwa wafuasi kuishambulia Marekani na washirika wake wa mataifa ya magharibi katika kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.

Vikosi maalum Marekani vilimuua babake Osama Bin Laden huko Pakistan mnamo 2011.

Aliidhinisha mashambulio dhidi ya Marekani mnamo Septemba 11 2001, ambapo takriban watu 3,000 waliuawa.

Hamza Bin Laden, anayeaminika kuwana umri wamiaka 30 alitangazwa rasmi na Marekani kama gaidi duniani miaka miwili iliyopita.

Amemuoa binti yake Mohammed Atta, aliyeiteka ndege mojawapo kati ya nne za abiia zilizotumika katika mashambulio hayo ya 2001, na kuivuruviza katika majengo ya World Trade Center mjini New York.

Barua kutoka kwa Osama Bin Laden zilizopatikana wakati makaazi yake yalipovamiwa huko Abbottabad alikouawa ziliashiria kwamba amekuwa akimpa Hamza mafunzo, anayeonekaana pia kama mwanawe kipenzi ili aichukue nafasi ya kiongozi huyo katika kundi la al-Qaeda, kwa mujibu wa wizara hiyo Marekani.

"Tunaamini huenda yupo katika mpaka wa Afghan-Pakistan na... atavuka kuingia Iran. Lakini anaweza kuwa sehemu yoyote... Asia ya kati kusini," samesema naibu waziri anayehusika na masuala ya usalama wa kidiplomasia Michael Evanoff.

Inaaminika Hamza Bin Laden ameishi na mamake nchini Iran, ambako inadhaniwa ndiko harusi yake ilikofanyika, huku taarifa nyingine zikiashiria huenda ameishi Pakistan, Afghanistan au Syria.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii