Edward Lowassa ambaye alipeperusha bendera ya CHADEMA katika nafasi ya urais arejea CCM

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa arejea CCM Haki miliki ya picha CHAMA CHA MAPINDUZI
Image caption Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania,Dr John Magufuli akimkaribisha Edward Lowassa

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa na aliyekuwa Mgombea wa urais kupitia tiketi ya CHADEMA katika Uchaguzi mkuu Uliopita amerejea CCM leo.

Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Mh. Edward Lowassa ametangaza kukihama Chama hicho na ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Lowassa ambaye alipeperusha Bendera ya upinzani mwaka 2015, alikuwa Kada wa chama hicho kwa miaka mingi kisha kukihama chama cha CCM baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wake.

Ni hatua iliyowashtua wengi kwani haikutarajiwa kutokana na mvutano uliokuwa hapo awali.

BBC imezungumza na katibu wa itikadi na uenezi, Humphrey Polepole na kusema Ndugu Edward amejiunga na chama cha CCM, alisema'' nimerudi 'nyumbani', . ''Lowassa alisema haoni haja tena ya kuwa mpinzani kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli ameona ajiunge na ccm ili awe sehemu ya kuendeleza gurudumu hili''.

Lowassa ajigamba upinzani unaimarika Tanzania

Shughuli ya kumpokea kwenye chama hicho zimefanyika katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho Dr.John Magufuli.

Lowassa alishaonekana mara kadhaa akikutana na Rais Dokta John Magufuli na kufanya naye mazungumzo katika Ikulu ya Tanzania huku Umma ukiwa haufahamu chochote kuhusu mazungumzo yao, Hatua ambayo ilizua minong'ono kuwa ana mipango ya kurudi CCM.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, kumekuwa na wimbi la wapinzani kuhamia CCM, hatua ambayo imeelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa upinzani unadhoofika.

Mada zinazohusiana