Kijana mdukuzi aliyelipwa dola milioni halali

Santiago Lopez akiwa amesimama kando ya magari yake mawili katika jimbo la Buenos Aires nchini Argentina
Image caption Santiago Lopez amejipatia utajiri kwa kudukua kwa njia iliyo halali kisheria

Kijana raia wa Argentina alianza kudukua kama njia ya kujifurahisha yapata miaka mitatu tu iliyopita , na akiwa hana mafunzo yoyote rasmi ameweza kutengeneza kitita cha dola $1.1m kwa njia ya kutafuta kasoro kidogo kidogo tu kwenye programu ya kompyuta zinazotumiwa na kampuni kubwa zaidi duniani.

Santiago Lopez amejinunulia magari mawili, jumba la kifahari lililopo ufukweni mwa bahari, na saa ya mkononi iliyotengenezwa na mbunifu wa mitindo ya saana heleni zake zinazoitwa 'bug bounty hunter'.

"Niliingia katika shughuli ya udukuzibaada ya kutizama sinema ya 'Wadukuzi'. Nilipenda filamu ya 'common lines' inayoelezea namna ya kufungua alama za siri kwa hiyo nikaanza kujifunza kupitia imtandao wa intaneti na nilifany autafiti kuhusu namna ya kutengeneza pesa kwa njia ya udukuzi, lakini wa unaokubalika kisheria."

Kenya yapoteza $40m kutokana na wadukuzi

Santi anasema anataka kuuonyesha ulimwengu kwamba wadukuzi sio lazima wawe ni watu wa kulaumiwa tu kama wanavyoelezewa katika vyombo vya habari.

Anakiri kuwa alishawahi kushawishika kutumia ujuzi wake kudukua kwa njia zisizofaa siku za mwanzoni, lakini anasema alivumbua programu ya 'Bug Bounty' uliomnusuru kujipata katika uhalifu .

Programu Bug bounty

Programu za Bug Bounty husaidia kuweza kudukua kwa njia za kisheria kwa kuwalipa wadukuzi kuweza kufanya jaribio kubwa kwenye mitandao kutokana na makosa.

Haki miliki ya picha Santiago Lopez
Image caption Santiago hutumia muda wake kuishi Buenos Aires na makao yake ya kifahari ya ufukweni

Huku udukuzi wa taarifa ama dataukiendelea kuwa kitu cha kawaida, makampuni yameanza kuwekeza zaidi kwenye bajeti zao za usalama.

Santi alitumia programu za 'Bug Bounty' kubwa zaidi duniani - HackerOne. Kwa miaka mitatu imekuwa ikiendelea ambapo wadukuzi wapatao 350,000 wamekwisha lipwa jumla ya dola milioni $45mkutoka kwa makampuni zikiwemo zile za Yahoo, Spotify, Airbnb, Adobe na Uber.

Jinsi wadukuzi walivyoiba bilioni 21 Kenya

Akiwa ndiye mdukuaji aliye juu kwenye chati ya wadukuzi, Santi amegundua zaidi ya alama za siri 1600 na amekuwa akipokea malipo ya mamia kadhaa ya dola, kulingana na umuhimu wa alama hizo.

" Nimeyasaidia mashirika mengi kama vile Twitter, Verizon, serikali ya Marekani na makampuni mengine mengi ambayo siwezi kuyazungumzia " Anasema Santiago

Kwa sasa Santiago ametulia kwani ni mmoja kati ya vijana wadogo walio tajiri zaidi nchini mwake na anawalipwa mara 40 ya wastani wa mshahara wa wazazi wake ambao wanajivunia sana mafanikio ya mtoto wao.

Haki miliki ya picha Santiago Lopez
Image caption Santi anataka kubadili mtazamo wa watu kuwahusu wadukuzi

Santiago akiwa ni kijana anayependa maisha ya kuvinjari, kufanya mazoezi ya mwili, anasema anauchukulia udukuzi kama kazi ya kawaida na anafurahia kubadili mtizamo juu ya wadukuzi.

Je tusome nini katika mgawanyiko ndani ya chama cha CUF Tanzania?

"Ni muhimu kwangu kwamba nina maisha yangu kama mimi na mimi ni wa kipekee. Si wadukuzi wote wenye nywele ndefu na wenye miwani wanaofanya mambo mabaya. kwa kila udukuzi wowote ninaoweza kuufanya , inteneti inaweza kuwa salama zaidi."

Anapokuwa hayupo katika jumba lake la kifahari kwenye ufukwe wa Argentine, Santi huwa anaishi nyumbani kwa wazazi wake mjini Buenos Aires.

Samaki wa kipekee aliyeonekana kwenye ufukwe wa California

Hufanya kazi kwa karibu saa nane kila siku, lakini udukuzi hufana zaidi nyakati za usiku.

"Wakati mwingine huwa ninafanyakazi hadi saa kumi za alfajiri nikidukua, ikimanisha kwamba ninalala mchana. Ninajaribu kutofanya masaa zaidi ya yale ninayohitaji kwasababu ninapenda kuwa na muda wa kufanya mambo mengine. Ni muhimu kutoka nje na kufanya vitu kama mazoezi ya mwili."

Santi anasema kwamba licha ya kupata umaarufu wa bug bounties, ataendelea kuwa mtu wa kawaida. Anatumai kutengeneza dola $500,000 mwaka huu.

"Ni mashindano," anasema. "Kuna wadukuzi wabaya kila mara wanaoangalia njia za kutengeneza pesa na kuiba data. Hatujashinda mbio hizi kwa sasa, lakini tumefikia kiwango cha 50/50."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii