Rais afanya mabadiliko serikalini wakati uhusiano wa Tanzania na baadhi ya nchi za magharibi unaonekana kutetereka.

rais Magufuli Haki miliki ya picha IKULU TANZANIA

Hatua ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kufanyia mabadiliko madogo baraza lake la mawaziri imeendelea kuzua maswali mengi nchini.

Mawaziri aliyowateua katika nyadhifa mpya walikuwa wachapa kazi katika wizara zao za awali.

Katika mabadiliko hayo, Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mahiga alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Haki miliki ya picha State House Tanzania

Wadadisi wanajiuliza mbona mabadiliko hayo yanafayika sasa?

Kiongozi wa chama cha Alliance for Change & Transparency,ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma amendika katika mtandao wake wa Twitter kuwa mabadiliko hayo ni hatua kubwa kwa Tanzania kuelekea kutiwa saini kwa mkataba wa kibiashara kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya na hali kadhalika kutolewa kwa nafasi ya mashauriano ya kisiasa

Fumbuka Ng'wanakilala, mwandishi wa habari, Tanzania anasema Balozi Augustine Mahiga ni mwanadiplomasia aliyebobea, lakini anaonekana kama ni mtu mpole.

Kwa upande wake Prof Palamagamba Kabudi, ambaye amewahi kuwa mwalimu wa sheria chuo kikuu, anaonekana ni mtetezi mahiri wa sera za serikali ya Rais John Magufuli.Mabadiliko haya madogo ya baraza la mawaziri yanakuja wakati uhusiano wa Tanzania na baadhi ya nchi za magharibi unaonekana kutetereka.

Haki miliki ya picha FOREIGN TANZANIA
Image caption Balozi Augustine Mahiga ni mwanadiplomasia aliyebobea, lakini anaonekana kama ni mtu mpole

Kabudi pia ameongoza mazungomzo kati ya serikali na wawekezaji wakubwa wa nje kama Barrick Gold Corp na Bharti Airtel ya India.

Kutokana na hilo inatarajiwa kama waziri mpya wa mambo ya nje, anaweza kuisaidia Tanzania kupata maelewano zaidi na nchi wafadhili.

Baadhi ya mabalozi wa nchi za magharibi hivi karibuni wameanza kutoa matamko hadharani kuhoji demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania.

''Namuona Profesa Kabudi kama mtu anayeweza kuwakumbusha hadharani pia mabalozi wa nchi za magharibi kuzingatia Mkataba wa Vienna na kutoingilia masuala ya ndani ya Tanzania''. ailsema Fumbuka Ng'wanakilala.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii