Mambo makuu aliyotaja Rais Magufuli kuhusu uwajibikaji wa Jeshi Tanzania

Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli Haki miliki ya picha Ikulu Tanzania
Image caption Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kuwajibika

Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kulinda heshima yake, kwa kufanya kazi zao kwa uaminifu.

Hafla ya kuwaapisha Waziri wa Katiba na Sheria Dokta Augustine Mahiga na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi ilifanyika baada ya rais Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri.

Mambo ambayo Magufuli aliyaibua kuhusu uchunguzi wa jeshi la polisi

Kuacha maswali mengi yakiwa hayajajibiwa.

Rais Magufuli amesema, kitendo cha Jeshi la Polisi kutotoa taarifa kuhusu hatua inazochukua kuhusu matukio yanayotokea huacha maswali mengi ambayo hukosa majibu

"Mnatakiwa muelewe kwamba Watanzania sio wajinga wanafahamu, natolea mfano tulipata stori nyingi za maelezo, wameteka wazungu lilipokuja kumalizika lile swala limekuja swali zaidi, yule aliyetekwa alikutwa Gymkhana, watu wanajiuliza alifikaje pale? Baadaye tunaona aliyetekwa anakunywa chai na Mambosasa (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam), maelezo hayapo,"Alisema Magufuli

Rais Magufuli amesema Watanzania walitaka kujua hatua ambazo Jeshi la Polisi ilizichukua kwa watu waliokamatwa wakihusishwa kuhusika na tukio hilo, ikiwemo mtu aliyekamatwa akidaiwa kuwabeba watuhumiwa waliomteka Mo Dewji.

Haki miliki ya picha Ikulu Tanzania
Image caption Dokta Augustine Mahiga akiapa kutumikia nafasi mpya ya Waziri wa katiba na sheria

"Watanzania walifahamu baada ya kushikwa aliyewabeba kesho yake angepelekwa mahakamani .''

Dosari ndogo ndogo zinalichafua Jeshi la polisi

Akirejea tukio la kutoroshwa dhahabu yenye thamani ya mamilioni ya fedha jijini Mwanza rais Magufuli amesema kuna ushahidi tosha kuwa polisi walihusika kwenye tukio hilo.

Amewataka makamishna na makanda wa jeshi la polisi kujenga sura nzuri ya Jeshi la polisi kama lilivyojengwa wakati huo na Hayati Mwalimu Nyerere.

''usiogope IGP kuleta majina ya makamishna mainspekta ambao unataka kupunguza nyota zao wala usisite, ambao wanashindwa kufanya kazi vizuri usimpeleke makao makuu , mpeleke akawe chini ya RPC mwingine.''

Hatua hii imepokelewa kwa hisia tofauti na watanzania, wengine wakiunga mkono kuwa itasaidia kurejesha uaminifu na nidhamu ndani ya jeshi la polisi lakini wengine wanaona kuwa Rais amechelewa sana kulisemea jambo hili kwa wakati huu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii