Kupandikiza chembe chembe hai katika mfupa huenda ikawa tiba ya Ukimwi

Mtu mmoja nchini Uingereza amekuwa wa pili kukutwa bila ya maambukizi aliyokuwa nayo awali ya HIV, baada ya kupandikizwa chembe chembe hai zinazokaa ndani ya mifupa ama celi - (Bone Marrow).

Madaktari wanasema mtu huyo aliyepewa jina la Mgonjwa London alipandikizwa chambe chembe hizo takriban miaka mitatu iliyopita na hajaonesha dalili za virusi hivyo kwa zaidi ya miezi 18, licha ya kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Mmoja wa madaktari waliohusika na matibabu yake hata hivyo ameonya kuwa ni mapema kuzungumzia tiba hiyo.

Mtu wa kwanza kuwekewa upandikizaji huo mjini Berlin Ujerumani, miaka 10 ilyopita kwa ajili ya kutibiwa Sareatani ya damu, ameendelea kuwa mzima wa afya bila ya maambukizo hayo.

Kufahamu zaidi upandikizaji huo unafanyika vipi, Mwandishi wa BBC Halima Nyanza amezungumza na Dokta Pius Muzzazi.