Fahamu vyanzo vya vifo vingi duniani?

watu Haki miliki ya picha Getty Images

Duniani kote , watu wana uwezo wa kuishi miaka mingi.

Mwaka 1950, wastani wa maisha ya binadamu duniani ilikuwa ni wastani wa miaka 46.

Baadhi ya mataifa , mchakato wa maisha huwa sio rahisi. Maradhi na matukio yasiyotarajiwa huwa yanakumbusha kwamba maisha yana ukomo.

Zipo sababu nyingi za vifo lakini vinavyotokea kwa sababu ya ugaidi, vita na majanga ya asili huwa havipungui 0.5% ya vifo vyote duniani.

Image caption Wastani wa maisha ya watu

Taarifa za watu kufa huwa zinategemea simulizi za namna vifo hivyo vinavyotokea na muda.

Sababu ya vifo duniani kote

Takribani watu milioni 56 duniani kote walikufa mwaka 2017.

Watu hawa ni milioni 10 zaidi ya watu waliokufa mwaka 1990, idadi ya watu duniani kote inaongezeka na watu uishi miaka mingi zaidi kwa wastani.

Zaidi ya watu asilimia sabini hufa kutokana na magonjwa yasioambukiza na ya muda mrefu. Magonjwa haya hayaambukizi kutoka kwa mtu na mtu na magonjwa haya huwa ya muda mrefu.

Ugonjwa ambao unaua watu wengi ni shambulio la moyo ambao unaathiri moyo na mishipa.

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na mshtuko wa moyo ni mara mbili na vinavyosababishwa na saratani, ugonjwa ambao ni wa pili kwa kusababisha vifo .

Ambapo kila vifo sita, kimoja kinakuwa kimesababishwa na saratani.

Magonjwa mengine ni kisukari ,magonjwa yanayoadhiri mfumo wa kupumua, ugonjwa wa akili pia upo kwenye orodha ya juu ya magojwa yanayosababisha vifo.

Namna gani vifo vinaweza kuzuilika

Jambo ambalo linastaajabisha ni idadi ya watu ambao wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika.

Takribani watu milioni 1.6 walikufa kutokana na ugonjwa wa kuhara mwaka 2017, na hii inaweka ugonjwa huo kuwa miongoni mwa sababu 10 zinazosababisha vifo.

Katika baadhi ya nchi , ugonjwa huo unauwa watu wengi zaidi.

Magonjwa ya ulemavu wa watoto unaosababisha vifo vya watoto chini ya siku 28 , ni sababu ya vifo milioni 1.8 mwaka 2017

Vifo vya mara kwa mara huwa vinatofautiana baina ya nchi na nchi.

Nchi ya Japan, watoto wapatao 1,000 wanakufa chini ya siku 28 baada ya kuzaliwa ukilinganisha na nchi 20 za nchi maskini .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Japan ni nchi ambayo watu wanaishi muda mrefu zaidi duniani

Magonjwa mengine ambayo yanazuiwa .

Ajali za barabarani zinasababisha vifo vingi katika nchi maskini na nchi tajiri, vifo milioni 1.2 vilisababishwa na ajali mwaka 2017.

Huku nchi ambazo zina watu wenye kipato kikubwa vifo vinavyotokea kwenye nchi hizo zinatokana na ajali za barabarani katika miongo ya hivi karibuni, lakini vilevile ajali hizo huwa ni za barabarani.

Hata hivyo, karibu mara mbili ya vifo vya watu vinatokana na watu kujiua au mtu na mtu kuuana.

Nchini Uingereza , vifo vya watu kujiua iko juu mara 16 , vifo hivyo ni vya watu wenye umri kati ya miaka 20-40.

Aidha kupungua kwa vifo vya watoto ,ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika huduma ya afya duniani.

Vilevile kuna mafanikio makubwa katika janga la magonjwa ya maambukizi kwa mfano janga la maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii