Zuckerberg: Aweka mipango ya kuboresha ulinzi wa siri za watumiaji wa Facebook

Zuckerberg Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg

Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa ana amini kuwa usalama wa huduma za ujumbe binafsi kupitia mtandao huo zitakuwa na umaarufu mkubwa kuliko soga za wazi ndani ya Facebook.

Zuckerberg ameelezea ndoto yake ya kufanya mageuzi ili kuwa na ulinzi mkubwa zaidi wa mawasiliano ya wateja wake na faragha zao.

Zuckerberg amesema kuwa Facebook na Instagram zimesaidia sana kuwaunganisha marafiki na jamii hivyo ameahidi kuleta mageuzi makubwa na kuufanya uga wake kuwa kama vile viunga vya miji ambapo watu hukutana ana kwa ana na kufanya mazungumzo.

Hata hivyo kufuatia ongezeko kubwa la watumiaji wa mtandao wake, amesema kuwa usiri na faragha za watumiaji wake ni linalotakiwa kuimarishwa.

Facebook imepitia vipindi vigumu na lawama kutoka kwa watumiaji wake kwa madai kuwa imekuwa ni moja ya mitandao ambayo ni rahisi kudukuliwa.

Mwaka 2018, kulikuwa na tuhuma kwamba taarifa za watumiaji wa mtandao wa Facebook wapatao million 50 ziliingiliwa na kutumiwa kwa maslahi ya kisiasa.

Ameongeza kuwa malengo mengine ya kuongeza usiri wa taarifa za watumiaji wa mtandao wake ni pamoja na kujiepusha kuweka taarifa muhimu ndani ya nchi ambazo zina udhaifu katika uhifadhi wa taarifa za mtandaoni na zile ambazo hazizingatii haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.

Haki miliki ya picha FACEBOOK

''Kwa misingi hii ni kwamba huduma zetu zitasitishwa katika baadhi ya nchi,huo ndiyo mpango uliopo kwa usalama wa watumiaji wetu''amfafanua Zuckerberg.

Mtandao wa Facebook umekuwa ukilaumiwa kukosa misingi mizuri ya uhifadhi wa siri wa watumiaji wake na kukosa namna ya kudhibiti taarifa za uongo zinazosamambazwa mtandaoni na hivyo kushindwa kuaminika.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii