Ligi ya mabingwa Ulaya : Manchester United yailaza Paris St-Germain 3-1

Diogo Dalot Haki miliki ya picha Getty Images

Kaimu meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameiongoza klabu hiyo kuingia katika robo fainali za ligi kuu ya mabingwa Ulaya katika usiku uliokuwa na msisimko mkubwa huko Paris na baadaye akatangaza: "Hichi ndichi tunachokifanya."

Romelu Lukaku alifunga mabao mawili kabla ya penalty ya Marcus Rashford iliotolewa kwa mfumo wa VAR kuchangia ufanisi huo wa United katika mabao waliofunga kwenye mechi za nje kwa gharama ya PSG.

"Ni klabu hii. ndicho tunachokifanya, hii ndio Man Utd," amesema Solskjaer, ambaye anasifika kwa kufunga bao la dakika mwisho kwa timu hiyo katika fainali ya mnamo 1999. "Hii ndio Champions League, ndicho inachofanya."

Hii ni mara ya kwanza tangu 2014 ambapo United imefuzu katika robo fainali. Timu za mwisho zitakazofuzu kwa robo fainali zitajulikana Machi 12 na 13 huku droo ikitarajiwa Machi 15.

"Tunaweza kwenda mpaka mwisho ," amesema Solskjaer. "Ndio tunajipendelea, blakini inabidi tusubiri droo alafu tucheze mchezo namna unavykuja."

Raia huyo wa Norway ameongeza: "Ni usiku wa kawaida kwa Manchester United. Tulikuwana mpango wa mchezo na imani kwa wachezaji ndiyo tulioitarajia. Kila mtu anahisi fahari kubwa".

Bao la utangulizi la Lukaku liliipatia United matumaini na licha ya kwamba Juan Bernat wa PSG alilisawazisha, Lukaku alitinga tena bao jingine katika nusu ya kwanza ya mechi kabla ya Rashford kuifunga siku kwa ushindi wa mashetani hao wekundu.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Ulikuwani mwanzo mzuri - tulipanga kufunga bao la kwanza lakini hatukulitarajia baada ya dakika mbili za kuanza mechi," Solskjaer amesema. "hilo liliweka wazi kwamba tutaka kufunga, mabao mengi.

"Tuliona katika mechi baina ya Real Madrid na Ajax, Barcelona dhidi ya PSG [mnamo 2017] - kuna hali ambazo zinafanana na inaonyesha kwamba akili ni muhimu katika soka.

"Vijana wetu ni wadogo na wenye umahiri, na ndico kilichotupatia ari na nguvu wakati tulipolihitaji bao."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii