Rais Kagame azuru Tanzania wakati uhusiano wake na Uganda ukilegalega

Rais Paul Kagame amekutana na rais John Magufuli katika ikulu ya Dar Es Salaam Haki miliki ya picha @UrugwiroVillage
Image caption Rais Paul Kagame amekutana na rais John Magufuli katika ikulu ya Dar Es Salaam

Rais wa Rwanda, Paul Kagame yuko nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Bwana Kagame ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuia ya Afrika mashariki (EAC) amekutana na rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania, John POmeb Magufuli katika ikulu mjini dar es Salaam.

Ziara yake nchini Tanzania imekuja wakati ambapo uhusiano wake na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ukilegalega huku mpaka kati ya Rwanda na Uganda ukifungwa.

Viongozi hao wamejadiliana masuala tofuati ikiwemo biashara na siasa.

Rais kagame alimshukuru mwenzake rais Magufuli, kwa ukarimu na ukaribisho mzuri kujadili masuala ya maendeleo baina ya matiafa hayo mawili ya Afrika mashariki.

'Kama kawaida Bwana rais, kila unaponikaribisha, napata fursa ya kuzungumza Kiswahili. Shukrani kwa nafasi hii kuniwezesha nikikumbuke kiswahili changu' alisema rais Kagame.

Alipowasili Alhamisi alasiri alipokelewa na waziri wa mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi.

Haki miliki ya picha @UrugwiroVillage

Viongozi hao wamejadili masuala mbali mbali kati ya nchi hizo mbili pamoja na ushirikiano wa kikanda. ilisema taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ya Tanzania.

Hatahivyo taifa hilo linajivunia uhusiano mzuri wa kibiashara na Tanzania.

Mara ya mwisho rais Kagame alizuru Tanzania ilikuwa mwezi Januari mwaka 2018 kwa ziara rasmi.

Mwenzake rais Magufuli ambaye hapendelei sana kusafiri nje ya nchi alizuru Rwanda mwezi Aprili mwaka 2016.

Ziara hii inafanyika katika wakati ambapo uhusiano wa Rwanda na nchi jirani Uganda umekuwa ukilegalega.

Mamlaka mjini Kigali zimekuwa zikilalamikia matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya raia wake wanaoenda Uganda.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii