Ikiwa leo wanawake wanasheherekea siku yao, Je kuna siku ya wanaume duniani?

An International Women's Day demonstration in Diyarbakir, Turkey in 2016 Haki miliki ya picha AFP

Inawezekana kuwa umesikia au kuona watu wanasheherekea siku ya wanawake duniani kupitia vyombo vya habari au umesikia kutoka kwa marafiki. Lakini ni kwa nini wanasheherekea?

Je siku hii ya wanawake ni sherehe au maandamano? Na je kuna sherehe kama hii kimataifa kwa ajili ya wanaume.

Ni zaidi ya muongo, watu duniani kote wamekuwa wakiadhimisha tarehe 8 machi kuwa ni siku ya kipekee kwa wanawake.

1. Namna gani siku hii ilianza?

Siku ya wanawake duniani imeanzia kwenye harakati za ajira mpaka ilipotambuliwa na Umoja wa mataifa kuwa siku maalum ya kuadhimisha katika mwaka.

Siku hii ilianza mwaka 1908, ambapo wanawake elifu kumi na tano waliandamana kutoka mji wa New York wakiwa wanadai muda wa kazi kupunguzwa, kulipwa vizuri na kuwa na haki ya kupiga kura.

Chama cha Socialist nchini Marekani ndio cha kwanza kutangaza kuwa siku hiyo ya wanawake kuwa ya kitaifa, baada ya mwaka mmoja.

Wazo la kuifanya siku hiyo kuwa la kimataifa lilitoka kwa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Clara Zetkin.

Mwanamke huyo alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa kuhusu wanawake wanaofanyakazi huko Copenhagen.

Ambapo kati ya wanawake 100 kulikuwa na wanawake 17 kutoka nchi mbalimbali ambao walikubaliana na wazo lake.

Siku hiyo ilisheherekewa kwa mara ya kwanza mwaka 1911, huko Austria, Denmark, Germany na Switzerland. Hicho mwaka huu ni mwaka wa 108, siku ya wanawake duniani inasheherekewa .

Haki miliki ya picha Topical Press Agency
Image caption Clara Zetkin muasisi wa siku ya wanawake 1910

Siku ya wanawake ilianza kusheherekewa rasmi na umoja wa mataifa(UN) mwaka 1975.

Mwaka 1996 ilikuwa sherehe ya kwanza ya wanawake iliyoangazia kusheherekea walikotoka na mipango ijayo.

Na mwaka huu kauli mbiu ikiwa 'Fikiria usawa, jenga umahiri na himiza mabadiliko'. Takwimu zinaonyesha kuwa nusu ya wanawake ambao wanafanya kazi wanawakilisha hamasa katika upande wa ajira duniani kote.

Siku ya wanawake duniani imekuwa ni tarehe ambayo inaonyesha namna wanawake walivyo katika jamii, siasa na uchumi, huku siku hii ikiwa inamaanisha kuwa inatoa hamasa na ueleo wa kuendelea kudai usawa.

2. Kwa nini Machi 8

Wazo la Clara kuhusu siku ya wanawake lilikuwa limelenga tarehe 8 Machi peke yake na hakukuwa na siku nyingine ya mbadala.

Siku hiyo haikuwa imepangwa rasmi mpaka vita ilipotokea mwaka 1917 wakati ambapo wanawake wa Urusi walikuwa wanadai mkate na amani na kujiingiza katika maandamano ya siku nne.

3. Je kuna siku ya wanaume kimataifa?

Siku ya wanawake ipo, na inasheherekewa tarehe 19 mwezi Novemba.

Lakini siku hii imeanza kusheherekewa tangu mwaka 1990 na haitambuliwi na Umoja wa mataifa (UN). Watu wanasheherekea siku hii katika zaidi ya nchi 60 na lengo la siku hii ni kuangalizia afya ya wanaume na wavulana , kuboresha uhusiano wa kijinsia ,kuhamashisha usawa wa kijinsia na kuangalia majukumu ya wanaume kama mfano wa kuigwa.

4. Namna gani wanasheherekea siku ya wanawake duniani?

Kimataifa ,siku ya wanawake ni siku ya mapumziko katika nchi nyingi ikiwemo Urusi ambapo biashara ya maua huwa inashamiri siku tatu au nne kuelekea Machi 8.

Haki miliki ya picha Getty Images

Nchini China, Wanawake wengi huwa wanapewa mapumziko ya nusu siku ingawa waajiri wengi huwa wahawawapi mapumziko hayo yaliyoamuriwa na serikali.

Marekani , mwezi huu wa tatu huwa unatambuliwa kihistoria kuwa mwezi wa wanawake.Rais hutoa tuzo kwa wanawake waliofanikiwa nchini humo.

5. Nini ambacho kinafanyika mwaka huu?

Mwaka huu , kampeni za siku ya wanawake duniani imechagua kuangalizia usawa wenye manufaa ambao unawahamasisha watu duniani kote kuchukua hatua katika kuweka usawa wa kijinsia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexandria Ocasio-Cortez amekuwa mwanamke mdogo wa kwanza kuchaguliwa na Congress mwezi Novemba mwaka 2018.

Kwa miezi 18 iliyopita, kumekuwa na harakati za wanawake katika mitandao ya kijamii wakiwa na mjadala wa mimi pia yaani 'hashtag #MeToo' wakizungumzia unyanyasaji dhidi yao wanaopitia katika maisha yao wakitaka mabadiliko.

Mjadala huo umeweza kuwa wa kimataifa na kujumuisha India, Ufaransa, China na Korea Kaskazini kutaka mabadiliko.

Marekani idadi ya wanawake waliochaguliwa iliongezeka . Wananchi wa Ireland wanataka katiba ibadilike na kuruhusu utoaji mimba uruhusiwe.

.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii