Rais asiyeonekana mbele za watu Abdelaziz Bouteflika atawezaje kuiongoza tena Algeria?

Abdelaziz Bouteflika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hotuba ya wazi inayofahamika kutoka kwa Rais Bouteflika ilikua mwaka 2014

Kwa raia wengi wa Algeria ni vigumu kuelewa ni kwa vipi rais wao mwenye miaka 82 ,aliyeugua kiharusi miaka sita iliyopita na kupata shida kwenye kutembea au kuzungumza anaweza kuongoza nchi.

Hakuna aliyeamini ilipotangazwa kuwa Abdelaziz Bouteflika anawania awamu ya tano mwezi Aprili-hata mwenyewe hakujitokeza binafsi siku ya Jumapili kujisajili kuwania nafasi hiyo .

Waalimu, wanafunzi, wanasheria hata waandishi wa habari waliingia mitaani kuandamana wakiwa na hasira , walionekana kutokubaliana na hatua ya kuongozwa na mtu ambaye haonekani.

Wengi wanahofu kuwa kutopatikana kwa mrithi wa Rais Bouteflika, ambaye aliingia madarakani mwaka 1999, kunaweza kusababisha hali ya usalama kuyumba nchini humo.

Kiongozi wa kwenye TV

Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchaguzi uliokuwa umetangulia.

Aliahidi kutekeleza suala la mgawanyo wa madaraka, kuupa nguvu upinzani na kuhakikisha haki za raia zinafuatwa.

Baadhi waliona kuwa hii ni ishara ya mabadiliko ya sera katika uongozi , lakini hakua ushahidi wa kuonekana kwake kwa muda mrefu.

Rais wa Algeria amtimua Waziri mkuu

Miss Algeria 'mweusi' abaguliwa

Raia wa nchi hiyo wamekua wakibahatika kumuona mara chache kwenye Televisheni akisalimiana na ujumbe kutoka nchi za kigeni wanaofika nchini Algeria.

Au kumuona kwenye ufunguzi wa mkutano mwaka 2016-akionekana amekaa kwenye kiti cha magurudumu, akionekana dhaifu, mwenye uchovu lakini mwenye tahadhari

Mpaka mwaka 2018,ikawa wazi kuwa Chama chake kimempendekeza kuwania tena uchaguzi wa mwaka huu.

Alikua kwenye ufunguzi wa Msikiti na vituo vya treni za umeme katika mji mkuu wa Algiers.Wiki chache baadae alikua kwenye ziara kutazama ujenzi wa Msikiti mkubwa wa tatu duniani uliogharimu dola za Marekani bilioni mbili.

Upinzani

Kiongozi huyo alishinda uchaguzi wa mwaka 2014, ingawa hakuwa na Kampeni zozote, mpaka sasa hana wapinzani wenye nguvu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Utawala wa Muammar Gaddafi nchini Libya ulionyesha kutoaminiwa baada ya kuruhusu mtu mmoja kutawala

Kwa nini sasa chama tawala na upinzani umeshindwa kupata wagombea wanaofaa

Upinzani una historia ya kugawanyika.Na chama tawala National Liberation Front kimetawala tangu Algeria ilipopata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1962 baada ya miaka saba ya vita vya nchini humo.

Wachambuzi wa siasa za nchini Algeria wanaona kuwa vijana wenye nguvu wananyang'anywa nguvu zao za uongozi na wazee.,Anaeleza mwandishi maarufu wa vitabu nchini Algeria, James McDougal kutoka chuo kikuu cha Oxford ameiambia BBC.

Amesema nchi imekabidhiwa mgombea ambaye ''yu karibu kufa''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji wakionyesha alama inayowakilisha Rais Bouteflika ambaye hutumia kiti cha magurudumu

Siku ya Jumapili,Rais Bouteflika kwa mara nyingine aliahidi kutoa nafasi ya kufanyika mazungumzo-na kusaidia mchakato wa mabadiliko ya katiba kwenye suala la duru ya pili ya uchaguzi.Ahadi hiyo ilikuja kwa mtindo wa barua iliyosomwa na mtangazaji kwenye kituo cha Televisheni cha taifa.

Kipya katika ahadi zake ni kuwa ataongoza mchakato wa uchaguzi ambao yeye mwenyewe hatashiriki.

Hiyo ingetoa fursa kuwahakikishia mbadilishano wa madaraka katika hali ya amani, haraka sana ikizingatiwa hali yake ya kiafya.

Lakini Algeria bado ina changamoto nyingi kuliko kile kinachoelezwa na waangalizi wa kikanda kuwa changamoto ni kubwa kuliko matatizo ya kiafya ya rais Bouteflika.

Mada zinazohusiana