Picha za satellite zinaashiria kuwa Korea Kaskazini inajiandaa 'kurusha' kombora

A satellite image shows the Sanumdong missile production site in North Korea on July 29, 2018. Haki miliki ya picha Reuters

Picha za Satellite kutoka kituo kimoja karibu na mji wa Pyongyang zinashiria kuwa Korea Kaskazini inajiandaa 'kurusha kombora' ama roketi.

Kumeripotiwa shughuli nyingi katika eneo linalofahamika kama Sanumdong, ambapo Korea Kaskazini huunganishia makombora na maroketi yake.

Mapema wiki hii ripoti ziliibuka kuwa Korea Kaskazini imejenga kituo kikuu cha kikuu cha kuundia silaha zake za nuklia.

Shughuli ya kubomoa kituo cha Sohae ilianza mwaka jana lakini ikasitishwa baada ya mazungumzo kati ya marais Kim Jong un na Donald Trump kuvunjika.

Siku ya Ijumaa rais Trump alisema atasikitika sana ikiwa Korea Kaskazini itarejelea tena kufanyia majaribio silaha zake hatari.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Trump amesema "Nitasikitika sana Korea Kaskazini wakifanyia majaribio silaha zao."

"Nitasikitika sana kuona wakifanyia majaribio silaha zao." alisema

Nini kinafanyika Sanumdong?

Magari makubwa yameonekana yakizunguka kituo cha silaha cha Sanumdong, hali ambayo siku zilizopita ziliashiriria kuwa Korea Kaskazini ilikuwa ikijiandaa kufyetua Kombora ama roketi kutoka eneo hilo.

Picha za satellite zimechapishwa na mitambo maalum ya Marekani inayofahamika kama NPR.

Mwandishi wa BBC mjini correspondent Laura Bicker amesema Korea Kaskazini huenda akaamua kuchukua hatua hiyo baada ya mazungumzo ya Hanoi kati ya Donald Trump na Kim Jong-un kumalizika bila kufikia muafaka wowote.

Ameongeza kuwa wataalamu wanahofia mitambo inayotumiwa kurusha silaha hizo hatari sio hasa kwa makombora ya masafa marefu.

Kulikuwa na matumaini kuwa viongozi hao wangelifikia mkataba wa kumaliza mzozo kati yao japo Korea Kaskazini ilikuwa tayari kupunguza shughuli zake za nuklia ikiwa Marekani ingeliondolea baadhi ya vikwazo dhidi yake.

Kituo cha kurusha makombora cha Sohae Tongchang-ri kimetumiwa kufanyia majaribio majaribio baadhi ya silaha zake lakini siyo makombora ya masafa marefu.

Wiki hii picha za satellite, kutoka vituo kadhaa vya Marekani na pamoja na ushahidi kutoka shirika la kijasusi la Korea Kusini, zilionesha ujenzi upya katika mitambo ya kurusha maroketi.

Haki miliki ya picha AFP

Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama nchini Marekani John Bolton, amesema kuwa Korea Kaskazini huenda ikawekewa vikwazo zaidi ikiwa itaendelea na mpango wake wa Nuklia.

Mkutano wa kwanza wa kihistoria kati ya Trump na Kim uliyofanyika mwaka 2018 nchini Singapore ulitoa matumaini ya uwezekano wa kukomesha mzozo katika rasi ya Korea.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii