Marekani yasisitiza ndege ya Boeing 737 Max 8 ni salama

Ndege ya kampuni ya ndege ya SilkAir ikiwa uwanjani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za sita za kampuni ya SilkAir aina ya Boeing 373 Max 8 zimeegeshwa kwenye uwanja wa ndege kwa sasa

Shirika la ndege la Singapore limesitisha kwa muda safari za ndege za Boeing 737 Max 8 zinazoingia na kutoka ndani ya nchi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa baada ya ndege ya kampuni ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing Max 8 kuanguka Jumapili, na kuwauwa watu 157 waliokuwemo.

Ilikuwa ni ajali ya pili iliyohusisha ndege ya aina hiyo katika kipindi cha chini ya miezi mitano iliyopita.

Uwanja wa Changi nchini Singapore ni wa tano wenye kuwa na shughuli nyingi zaidi duniani na kiituo kinachounganisha safari nyingi za kutoka bara Asia hadi Ulaya na Marekani.

Utawala wa Mamlaka ya safari za anga la Marekani ameziambia kampuni za ndege kuwa anaamini ndege za Boeing 737 Max 8 zinafaa ,baada ya ajali mbili zilizosbabisha vifokatika kipindi cha miezi takriban sita.

Haki miliki ya picha JONATHAN DRUION
Image caption Ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi

Ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi ilianguka dakika sita baada ya kuondoka uwanjani Jumapili na kuwauwa watu 157 waliokuwemo ndani yake.

Tukio hilo lilifuatia ajali nyingine ya ndege Lion Air 737 Max 8 iliyoanguka mwezi Oktoba na kuwauwa watu 189.

Baadhi ya mamlaka za ndege zimetoa wito ndege hiyo izuwiwe kusafiri hadi uchunguzi kamili utakapo kamilika.

Lakini Jumatatu jioni , Mamlaka ya safari za ndege ya Marekani (FAA) iloitoa taarifa inayoelezea namna ndege hiyo inavyofaa, ikisema ni salama kupaa

China, Indonesia, Singapore, Australia, Uturuki na Ethiopia zimekwisha tangaza kusitishwa kwa safari za ndege hiyo.

Argentina, Mexico na Brazil wameahirisha safari hizo

Haki miliki ya picha FlightRadar24

Lakini ni makampuni machache tu ya ndege yanayotumia Boeing Max 8 kutoka na kuingia nje ya nchi.

Makampuni kadhaa ya ndege na wasimamizi wa viwango vya ndege duniani wamepiga marufuku utumiaji wa ndege aina ya Max 8 kufuatia ajali ya ndege za ndege hiyo.

Singapore inaaminiwa kuwa nchi ya kwanza kupiga marufuku safari za ndege za aina ya Max.

Je kuna uwezekano wa kuvurugika kwa safari?.

Mamlaka ya safari za ndege ya Singapore imesema safari zilizoathirika ni za kampuni ya ndege ya SilkAir, inayotumia ndege sita za Boeing 737 Max 8 , pamoja na zile za China Southern Airlines, Garuda Indonesia, Shandong Airlines na Thai Lion Air.

Imesema inashrikiana na ndege nyingine pamoja na uwanja wa ndege wa Changi ili kupunguza athari kwa wasafiri. Wataalamu wameiambia BBC kuwa uwezekano wa kuvurugika kwa safari upo.

Haki miliki ya picha JONATHAN DRUION
Image caption Ndege aina ya Boeing 737 iliyoanguka Ethiopia Jumapili

Hata hivyo mshauri wa safari za anga Ian Thomas alisema: " Ni wazi uamuzi huo utasababisha kufutwa na kuvurugika kwa mpango wa safari kwani wasafiri watabadilishiwa ndege kama zitakuwepo."

Mwandishi wa BBC aliyeko kwenye uwanja wa ndege wa Changi ameelezea kuwepo kwa mkanganyiko.

Baadhi ya safari za ndege zimefutwa, lakini haijabainika ikiwa kuahirishwa kwa safari za Boeing 737 Max 8 ndio sababu.

Image caption Captain wa ndege ya Boeing 737 iliyoanguka nchini Ethiopia Yared (kulia) akiwa pamoja na wahudumu wa ndege wa Ethiopian Airlines

Nchini Marekani utawala wa shirika la ndege nchini humo (FAA) limeyaambia mashirika ya ndege kuwa linaamini aina ya Boeing 737 Max 8 inafaa kwa safari za anga licha ya kupata ajali mbili zilizowauwa mamia ya watu.

Mwezi October mwaka jana Lion Air Boeing 737 Max ilianguka muda mfupi baada ya kuondoka kutoka Jakarta, Indonesia, na kuwauwa watu wote 189 waliokuwa ndani yake.

Ndege ilikuwa imetumika kwa safari za usafiri kwa chini yamiezi mitatu.

Ndege ya Ethiopia ET302 pia ilianguka chini dakika chache tu baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege.

Haki miliki ya picha ETHIOPIAN AIRLINES
Image caption Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya thiopian Airlines Tewolde Gebremariam akiwa kwenye eneo la tukio la ajali ya ndege Jumapili

Ndege iliyokuwa na nambari ya usajiri ET-AVJ - ilipaa angani kwa mara ya kwanza Oktoba 2018.

Utofauti wa ndege hiyo na muundo wa awali

Mchambuzi wa safari za ndege aliyeko Jakarta Gerry Soejatman ameiambia BBC kuwa ''injini ya 737 Max iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake ,ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing . Hilo linaathiri mizani ya ndege''

Kamati ya usalama wa safari za taifa nchini Indonesia imebainisha kuwa safari za ndege za Lion Air 610 zilikuwa na hitilafu iliyotokana na moja ya kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kumpatia rubani isharawakati ndege inapokuwa katika hatari ya kuanguka.

Uchunguzi kuhusu hitilafu hizo bado haujafikia matokeo ya mwisho juu ya chanzo cha mkasa.

Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu ya software inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boieng 737, lakini marubabi hawakuwa wameambiwa told that.

Image caption Captain wa ndege ya Boeing 737 iliyoanguka nchini Ethiopia Yared (kulia) akiwa pamoja na wahudumu wa ndege wa Ethiopian Airlines

Katika kipindi cha siku chache baada ya ajali ya Lion Air, watengenezaji wa ndege ya Boeing walitoa muongozo wa namna ndege zinavyopaswa kuendeshwa.

Mwaka 2017 Boeing iliuza ndege 763, idadi ambayo imetajwa kuwa ya juu zaidi kuuzwa ndani ya mwaka mmoja.

69% ya ndege hizo ilihusisha uuzaji wa kwanza wa ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX ambazo ziliwasilishwa kwa mashirika 17 tofauti ya ndege duniani.

Ndege zote za 737 MAX zilizouzwa zinaweza kutambuliwa kupitia nambari maalum 'B38M'.

Mauzo ya kampuni ya kuunda ndege ya Boeing ilipanda kwa 31% mwaka huu.

Kampuni hiyo ilipata faida ya zaidi ya dola bilioni $100 kwa mara ya kwanza katika historia yake ya miaka 102 baada ya kuongeza uuzaji wa ndege za kibiashara na za kijeshi.

Licha ya ufanisi huo wa kibiashara kampuni ya Boeing imejipata katika njia panda hasa baada ya ajali ya ndege zake mbili zilizopata ajali chini ya miezi mitano.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii