Afrika mashariki impokee vizuri Macron, , wasema wachumi

Rais Emmanuel Macron
Image caption Rais Emmanuel Macron anatarajia kuisaidia Kenya kujenga usafiri wa leri ya kasi kutoka kati kati mwa mji wa Nairobi hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye anafanya ziara katika mataifa ya Afrika, leo anatarajia kuhudhuria kikao cha mazingira cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya.

Anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu mjini Nairobi na kuisaidia Kenya kujenga usafiri wa leri ya kasi kutoka kati kati mwa mji wa Nairobi hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Macron anataka kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kijeshi na kitamaduni na mataifa ya Afrika, lakini anafahamu fika kwamba kuwa anaingia Afrika wakati mataifa mengine kama vile Uchina yamekwishaimarisha ushirikiano wake na mataifa mbali mbali ya Afrika katika nyanja zote ikiwemo biashara, siasa na uchumi uhusiano ambao unaendelea kupanuka.

''Ufaransa imechelewa sana kuwa na ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi na mataifa ya Afrika Mashariki'', ameiambia BBC mchambuzi wa masuala ya kiuchumi Profesa Ibrahim Lipumba Jumatano.

Ameongeza kuwa, miaka 10 iliyopita nchi hiyo ilipoteza ushawishi wake kw amataifa ya Afrika ambao ulichukuliwa na mataifa kama vile Uchina, India na Marekani na hivyo kwa sasa ni nchi inayochukua nafasi ya saba kwa biashara mataifa ya Afrika kwa ujumla, na sasa inataka kubadili hilo kw akujiimarisha zaidi kibiashara na kiuchumi katika bara hili.'', alisisitiza Profesa Lipumba.

Ufaransa ni mshirika mzuri wa kiuchumi na Afrika mashariki?.

Kulingana na mchambuzi wa masuala ya kiuchumi Profesa Ibrahim Lipumba, mataifa ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla yanapaswa kuipokea Ufaransa kama mshirika wa kibiashara na kiuchumi.

Anasema, kinyume na ilivyokuwa wakati wa vita baridi vya dunia, nyakati hizi Afrika haipaswi kuchagua ni nani wa kufanya nae biashara.

''Tunapaswa kufanya biashara na yeyote anayekuja upande wetu, viongozi wa Afrika wampokee vizuri Macro kuangalia ni fursa zipi za kiuchumi na kibiashara alizonazo kwa nchi zao''. Amesema.

Image caption ''Ufaransa imechelewa sana kuwa na ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi na mataifa ya Afrika Mashariki'' amesema Profesa Ibrahim Lipumba

Ufaransa ni kama mshirika wa biashara na uchumi.

Ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kushirikiana kibiashara na Ufaransa, kutokana na kwamba ni miongoni mwa mataifa yenye ushawishi wa kibiashara na kiuchumi miongoni mwa mataifa ya Ulaya.

Kwa ushirikiano mwema na Ufaransa Afrika itaweza kujenga mahusiano mema na mataifa mengine ya Ulaya kibiashara na kiuchumi.

Emmanuel Macron anaizuru Kenya baada ya kufanya ziara katika mataifa ya Djibouti na Ethiopia Jumanne, ambapo aliahidi kuwa na uhusiano wa "kuheshimiana "

Akiwa Ethiopia alisaini mkataba mpya wa ulinzi na Ethiopia na anatarajiwa kusaini mkataba wa ujenzi wa leri itakayotoka kati kati mwa mji mkuu wa nchi hiyo Nairobi kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatano.

Macron aliielezea Djibouti, ambalo ni koloni la mwisho la ufaransa iliyopata uhuru wake 1977 kama "mshirika wa kihistoria na wakimkakati".

Kwa pamoja Serikali za Paris ana Beijing -- pamoja na Japan, Marekani zina vituo vyake vya kijeshi have nchini Djibouti kutokana na mahali ilipo ambako ni mapito ya meli zinazoelekea kwenye mfereji wa Suez.

Haki miliki ya picha OFFICE OF THE PRIME MINISTER ETHIOPIA
Image caption Waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed akimpokea mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Adis Ababa

Umuhimu wake wa kijiografia katika eneo la upembe wa Afrika ni msingi matumaini ya taifa la Djibouti la kuwa kituo kikubwa cha biashara.

Miaka miwili iliyopita, taifa hilo dogo zaidi Mashariki mwa Afrika lilizindua bandari kubwa zaidi, ikiwa ni sehemu ya upanuzi wa miundombinu na sehemu ya ujenzi wake ilifadhiliwa na Uchina, kama vile bandari nyingine tatu na leri inayoelekea katika nchi jirani ya Ethiopia.

Inairuhusu Uchina kuifikia Afrika na Ulaya kupitia bahari ya Hindi.

Akiwa nchini Ethiopia Macron alitembelea mji uliopo mbali nchini Ethiopia wa Lalibela unaofahamika kama kituo cha kihistoria kutokana na makanisa ambayo yalijengwa karne ya 13, yanayotambuliwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano

Aliahidi ''kugharimia kifedha na kusaidia shughuli za Waethiopia za ukarabati wa makanisa", yanayotishiwa na mmmonyoko ambayo kwa sasa yamefunikwa na mabati.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, Macron pia alitangaza makubaliano ya kijeshi ambapo Ufaransa itatoa mkopo wa dola milioni 96 kwa Ethiopia kwa ajili ya kusaidia kuanzisha jeshi la majini kwa ajili ya taifa hilo lisilopana na bahari.

Wakati wa ziara yake Ethiopia, Rwanda ilimualika kuhudhuria maadhimisho ya 25 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimari ya mwaka 1994 yaliyoweauwa watu 800,000.

Kwa muda mrefu maafisa nchini Rwanda wamekuwa wakiishutumu Ufaransa kwa kuhusika katika mauaji hayo.

Macron hajaonyesha ikiwa atahudhuria kumbu kumbu hizozinazofanyika tarehe 7 April kila mwaka mjini Kigali au la.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii