Familia zaombeleza mkasa wa ajali ya ndege Ethiopia
Huwezi kusikiliza tena

Hussein Swaleh: Familia zaomboleza ajali ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing 737

Taarifa ya shirika la ndege la Ethiopia imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw.

Wakenya 32 walikuwa miongoni mwa watu 157 waliofarika ajali ya ndege ya Ethiopia.

Mmoja wa waliofariki katika ajali hiyo ni katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka nchini Kenya, Hussein Swaleh.

Mwandishi wa BBC Roncliffe Odit amezungumza na mtoto wake Feisal Hussein Swaleh.