Tani 11 za Samaki zilizoingia kwa njia za panya kutoka China zateketezwa Tanzania

Samaki aina ya Sato Haki miliki ya picha FAO
Image caption Samaki waliingizwa Tanzania bila kuwa na viambatanisho vyovyote

Tani 11 za samaki aina ya Sato zimeteketezwa baada ya kubainika kuwa wana vimelea vya sumu.Samaki hao ambao wanaripotiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka nchini China wana thamani ya dola za Marekani 33,000

Waziri wa mifugo na uvuvi nchini Tanzania, Luhaga Mpina amesema watu walioingiza samaki hao nchini walitumia njia zisizo halali.

Samaki hao walitelekezwa baada ya mamlaka kukamata shehena hiyo, Kama ilivyo ada samaki hao walipitia kwenye vipimo kabla ya kuamuliwa kupigwa mnada, ndipo walipobaini kuwa samaki hao wana kiwango kikubwa cha kemikali ya Zebaki ambacho ni hatari kwa matumizi ya binaadamu.

Aina nyingine ya sumu iliyopatikana kwenye samaki ni viatilifu vya DDT.

Mamlaka zimetahadharisha watu kutofanya biashara kinyume cha taratibu kuepuka kufilisiwa na upoteza mitaji yao,

Papa kutibu binadamu saratani na 'uzee'

Sababu ya kukamatwa kwa shehena ya Samaki

Kutokuwepo kwa nyaraka zinazo onyesha kama samaki wameidhinishwa kuingia nchini kutoka kwa mamlaka ya nchi walikotoka

Nyaraka kuonyesha kuwa wamezalishwa au kuvuliwa kwa njia halali huko walikotoka.

Kutoonyesha samaki wamezallishwa na kiwanda kilichoidhinishwa na nchi husika kufanya shughuli za uzalishaji au uvuvi

Kutokuwepo kwa Nyaraka kuonyesha kuwa samaki ni salama ili kulinda afya ya mlaji

Kasha kutoonyesha alama ya kuonyesha jina la muagizaji wa samaki

Wizara imesema samaki hao wangesababisha hatari kubwa kwa walaji, madhara ambayo yangejitokeza siku za usoni kama vile maradhi ya saratani, matatizo katika mfumo wa uzazi na watoto kuzaliwa wakiwa na matatizo ya akili.

Mada zinazohusiana