Wanawake Tabora watumia ugoro kupunguza matamanio
Huwezi kusikiliza tena

Tabora: Wanawake wa Urambo watumia ugoro kama njia ya kupanga uzazi na kupunguza hamu

Baadhi ya wanawake mkoani Tabora nchini Tanzania wanatumia ugoro (tumbaku iliyosagwa) kupunguza hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya wanaotumia njia hii ni wale ambao wametengana ama wamefiwa na waume zao ama kuwa mbali kwa kipindi kirefu.

Hakuna utafiti wa sayansi kufikia sasa uliofanywa kuthibitisha kwamba kweli ugoro unasaidia kupunguza hamu au ina faida katika njia za upangaji uzazi.

Lakini Je madhara yake ni yapi?

Mwandishi wa BBC Eagan Salla alitembelea Kijiji cha Ugala wilayani Urambo Mkoani Tabora