Namna gani utaweza kuondoa hofu ya kusafiri kwa kutumia ndege

Mwanamke akiwa mwenye wasiwasi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kwa watu wengine, kuwa ndani ya ndege kunasababisha hofu

Huwa unatoka jasho jembamba kwenye viganja unapokua ndani ya ndege tayari kuanza safari? huwa unashikilia kwa nguvu mikono ya kiti wakati Ndege inapopaa? huwa unasikia mapigo ya moyo yanakwenda mbio unapokaribia kutua?

Ikiwa ndivyo kama ilivyo asilimia 17 ya wamarekani (kwa mujibu wa Boeing) wanaweza kuwa na hofu ya kuruka na ndege.

Baada ya ajali ya hivi karibuni ya ndege ya shirika la Ethiopia , iliyosababisha vifo vya watu 157 ni hofu inayoeleweka.Lakini ajali za ndege hutokea kwa nadra.

Inakadiriwa kuwepo kwa ndege takribani 37,800,000, kiwango cha ajali ni takriban tukio moja kwa kila ndege 2,520,000 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mtandao wa usalama wa anga (ASN)

Lakini kwa kuwa ajali za ndege huripotiwa kwa kiasi kikubwa, hofu zetu huongezeka.

bahati tu, hofu ya kusafiri kwa ndege inaweza kutiba-kuna namna nyingi ya kuondokana na hofu.Hapa wataalamu wanatoa ushauri

Zoezi la kuvuta pumzi na kuachia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanasaikolojia Matthew Price anasema kuvuta pumzi ndani ya ndege kunafanya hofu kutoweka

Kuna watu wanaoogopa kuruka na ndege kwa sababu ni mara yao ya kwanza kupanda ndege, au walikutana na jambo lililowatatiza waliposafiri awali, Mtaalamu wa masuala ya saikolojia katika chuo cha Vermont, Matthew Price anaeleza.

Kampuni ya Boeing yasitisha matumizi ya ndege zote za 737 Max

''Kwa bahati mbaya hakuna maelezo kuhusu sababu ya mtu kuwa na hofu hiyo, lakini kuna sababu muhimu nyingi,'' aliongeza.

Price anasema zoezi la kuvuta pumzi-vuta pumzi taratibu kupitia mdomoni na taratibu uitolee puani-wakati mwingine fanya hivyo mara kadhaa inaweza kusaidia.

Tiba

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuongelea hofu inayokukabili inasaidia

Baadhi yetu huvaa vifaa vya kusikilizia muziki masikioni ili zitusahaulishe, wengine hunywa dawa za kuwalaza usingizi, au za kuwaondolea wasiwasi -wengi pia hunywa pombe

lakini ikiwa hofu itakufanya ushindwe kabisa kupanda ndani ya ndege, kuna tiba ambayo inaweza kusaidia.

Tiba dhidi ya matatizo ya hisia za uoga, tiba ya kisaikolojia, tiba ya utambuzi wa tabia zote zimekua zikitumika kupambana na hofu ya kuruka na ndege.

Kabili hofu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption NJia ya kuvaa Kifaa kinachokuonyesha uhalisia hukuondoa hofu

Wataalamu wanasema njia nzuri ya kuondokana na hofu ni ''kukabiliana na hofu'', kidogo kidogo unapojizoeza kuruka na ndege mara kwa mara kwa msaada wa uangalizi wa daktari.

kuna mafunzo maalumu ya kama ya ''kuruka na ndege bila hofu'' programu inayotolewa na taasisi ya Virgin Atlantic.Inahusisha marubani ambao hujibu maswali na kueleza mambo yanayokwenda sambamba na hofu ya kuruka na ndege kama vile kufahamu ukweli kuhusu namna ambavyo ndege huruka, mashirika yanafanya nini kupambana na vitendo vya kigaidi, na vitu ambavyo marubani hufanya pakitokea hitilafu kwenye injini.

Mtaalamu Barbara Rothbaum anasema ''93 ya watu wamekuwa katika hali zao za kawaida baada tu ya vipindi vinane vya mafuzo hayo na kuanza kupanda ndege'', anaeleza.

vipindi vinne vya kwanza vilifundisha watu njia za kudhibiti hofu, anaeleza,kwa mfano, jinsi ya kutambua mawazo hasi (kwa mfano, ''tutapata ajali'',) na kuyasahihisha.

vipindi vinne vya mwisho ni kutumia uhalisia kusaidia watu kukabili hofu kwa kutumia tiba ili hofu iweze kupungua.

Matumaini ni kuwa vipindi hivi husaidia kutoa uelewa, na hatimaye kudhibiti hofu,wazo ni kuwa ukielewa jambo, haliwezi kukusumbua.

Jua uhalisia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwaka 2017 ulikua mwaka wa kihistoria kwa usalama wa ndege za kibiashara

Ajali za ndege hufanya habari kuwa kubwa ana.hasa hii ya karibuni iliyohusisha ndege ya Boeing 737 Max iliyoanguka dakika sita baada ya kuruka kutoka Addis Ababa.Watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walipoteza maisha.