Kenya: Evelyn Namukhula, mama aliyejifungua watoto watano kwa mkupuo

Bi Evelyn Namukhula Haki miliki ya picha KWA HISANI
Image caption Bi Evelyn Namukhula na mumewe wana jumla ya watoto tisa sasa

Kupata mtoto kwa kawaida ni neema na majaaliwa ya mwenyezi.

Na kama ni baraka basi Bi Evelyn Namukhula kutoka eneo la Kamamega nchini Kenya ilikuwa ni kubwa.

Bi Namukhula alijifunga watoto watano kwa mkupuo katika hospitali kuu ya Kakamega Jumatano tarehe 13 Machi mwaka huu.

​Mama huyo mwenye umri wa miaka 28-alijifungua kwa upasuaji ambapo alipata watoto wa kike wawili na wavulana watatu wote wakiwa salama.

Haki miliki ya picha KWA HISANI
Image caption Bi Evelyn Namukhula kulia akiwa hospitalini pamoja na daktari na wauguzi wa hospitali kuu ya Kakamega magharibi mwa Kenya

NamuKhula na mumewe Herbert Wawire, ambaye ana ulemavu wa kutosikia kwa sasa wana jumla ya watoto tisa.

Si mara ya kwanza kwa mwanamke kujifungua watoto zaidi ya watatu katika eneo la Afrika Mashariki.

Nchini Tanzania Radhia Solomon mkazi wa dar es salaam alijifungua watoto wanne.

Haki miliki ya picha KWA HISANI

Mwezi September 2018, baba wa mapacha mwenye umri wa miaka 28 alizimia katika hospitali baada ya kupata habari kuwa mkewe, Jacinta Mwihaki, amejifungua watoto watatu.

Francis Gitau anasema aliwapokea watoto watatu kwa furaha iliyojaa hofu juu ya namna atakavyowalea kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyopo.

Gitau na mkewe Jacinta Mwihaki, mwenye umri wamiaka 30, walikuwa tayari wana mapacha wenye umri wa miaka minne.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii