Samora Mangesi: Mtangazaji wa Afrika Kusini aliyeumizwa kwa ubaguzi wa rangi

Samora Mangesi alituma picha yake akiw ana majeruhi upitia tweeter akidai ameshambuliwa na kuumizwa Haki miliki ya picha Samora Mangesi
Image caption Samora Mangesi alituma picha yake akiw ana majeruhi upitia tweeter akidai ameshambuliwa na kuumizwa

Mtangazaji wa Televisheni na redio nchini Afrika Kusini mweusi amesema kuwa amekuwa muathiriwa wa shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangibaada ya kusimamisha gari lake kwa ajili ya kulisaidia kundi la wazungu ambao gari lao lilikuwa limepinduka.

Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata kaika kile alichodai ni shambulio , analosema lilifanyika Ijumaa.

Yeye na marafiki zake wawili wa kike waliitwa "nyani", alisema.

Walipoulizwa ni kwanini wanatukanwa, walipigwa hadi wakapote zafahamu.

Wakati wa tukio hilo lililotokea mjijni, Mangesi, ambaye ni mtangazaji wa shirika la habari la Afrika Kusini ABC, alisema kuwa alipata majeraha usoni mwake na mwili wake ulikuwa na damu baada ya kupigwa mateke alipokuwa amelala chini.

"Hata wakati nilipokuwa nikiwekwa kwenye gari la wagonjwa, mmoja wa jamaa hawa alijaribu kupita juu ya mwili wa mmoja wa rafiki zangu na gari yake aina ya pick-up ikabidi madaktari waingilie kati ." Alieleza Mangesi.

Siku zilizofuata baada ya shambulio hilo, kumbu kumbu yake iliathirika sana ", alisema.

"Licha ya kwamba walisema nilizinduka , sina kumbu kumbu nikiwa ndani ya gari la wagonjwa, nilivyofika hospitalini na hata sikumbuki mengi kuhusu matibabu yangu ."

Alifikiria juu ya "kusahau yaliyompata na kuendelea na maisha yake", lakini sasa ameripoti tukio hilo kwa polisi , aliongeza.

Taarifa juu ya shambulio hilo zimezua hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na huku wakiitaka polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii