Kwanini Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanahitaji kushindana kuendeleza uhasimu mkubwa?

Lionel Messi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lionel Messi amefunga mabao 62 goals katika mechi zake 61 kwenye ligi kuu ya mabingwa huko Camp Nou Barcelona

Unachoweza kufanya, naweza kukifanya vyema zaidi.

Usiku baada ya Cristiano Ronaldo kutinga hat-trick kuchangia ushindi wa Juventus dhidi ya Atletico Madrid na kufuzu kwa robo fainali katika ligi kuu ya mbingwa, hasimu wake wa jadi Lionel Messi amefuata mkondo kwa machango mkubwa ulioipa ushindi Barcelona dhidi ya Lyon kwa mabao 5-1.

Ukitathamini, Messi alifanikiwa pia kumpiku Ronaldo kwa kutoa mabao manne: mawili aliyoyafunga mwenyewe, na mengine mawili aliyotoa pasi safi kwa Gerard Pique na Ousmane Dembele.

Ushindi huo unairuhusu Barca kuendelea kuipeperusha bendera ya La Liga kama wawakilishi wa pekee wa Uhispania katika timu nane za mwisho pamoja na kumpa fursa zaidi Messi kutimiza ahadi yake - aliyotoa katika hotuba kwa mashabiki kabla ya msimu kuanza - kulileta taji la Ulaya kwa mara ya kwanza tangu kushuhudiwa 2015.

Na kwa kweli, inaendeleza pia uhasimu mkubwa katika historia ya soka kuwahi kushuhudiwa.

Je Messi na Ronaldo wanahamasishana?

Haki miliki ya picha BBC Sport

Iwapo hapangekuwa na Cristiano Ronaldo, je Lionel Messi angemuunda?

Suala la kiasi gani wachezaji hawa wawili wanavyohamasishana ni la kuvutia sana, na ni rahisi mtu kumfikiria Messi akiwa amekaa nyumbani Jumanne usiku akimtazama Ronaldo akiiangamiza Atletico kwa mabao, akitazama televisheni kwa hasira na kukasirika huku pengine akisema: "Nitamuonyesha!"

Licha ya kwamba ni picha ya kuvutia kuifikiria, hatahivyo huenda sio ukweli - angalau kwa mtazamo wa Messi.

Huenda atalionyesha katika namna tofauti, lakini Messi ana umahiri kama alivyo nao Ronaldo. Kando na magoli na ushindi binafsi, lakini uraibu wa mchezaji huyo wa Argentina ni mataji.

Ronaldo, tunaweza kusema, haonekani kuwa na furaha akiwa uwanjani, hadi iwapo ametinga goli - na hata hapo furaha hiyo haidumu kwa muda mrefu, kwasbaabu anataka kufunga bao jingine tena.

Na uraibu huo wa kufunga mabao imekuwa na mchango mkubwa katika ufanisi wake katika kucheza soka ya kulipwa.

Messi, hatahivyo, ni tofuati, anafahamika kwa kuwa mkarimu kwa kutoa pasi kwa wachezaji wenzake hata kama ana nafasi ya kutinga bao yeye mwenyewe.

Na pia husherehekea bao kwa kumgeukia mchezaji aliyempa pasi nakumpa tabasamu la asante.

Haki miliki ya picha EPA

Badala ya kuwa bora kuliko Ronaldo, motisha kuu kwa Messi - kwa mujibu wa watu walio karibu naye ni kuwa Messi bora zaidi na kushinda mataji mengi iwezekanavyo.

Messi na Ronaldo kuwa na ushindani mkubwa baina yao ni hadithi nzuri kwa mashabiki kujadili na vyombo vya habari kuripoti, lakini huenda sivyo inavyodhaniwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii