Zoezi la uokoaji laendelea Lagos, watu 50 wapatikana hai, 11 wakiwa wamepoteza maisha

waokoaji wakiwa kazini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waokoaji wakiendelea na kazi ya kuwapata watu walionasa kwenye kifusi

.Wafanyakazi wa huduma za dharura mjini Lagos wanaendelea na kazi ya kuokoa maisha ya watu kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoanguka siku ya Jumatano katika eneo la Ita-Faaji , Mji wa kibiashara.Polisi iliithibitishia BBC kuwa mpaka sasa watu 50 wameokolewa huku wengine takribani 11 wamepoteza maisha

Serikali jijini Lagos imesema uchunguzi utafanyika baada ya operesheni ya ukoaji kukamilika na kuhitimisha kuwa wale wote waliohusika watashtakiwa.

Ni vigumu kufahamu idadi kamili ya waliokuwa ndani ya jengo kwa sababu ni jengo lililokuwa likitumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo shule iliyokuwa na wanafunzi 100, ghorofa ya katikati kulikua na makazi ya watu wakiishi na familia zao na chini ya jengo kulikua na maduka ambayo wafanyabiashara walikua wakifanya biashara zao.

Kuna rais na mama wa taifa bandia Nigeria?

Jeshi la Nigeria lavamia ofisi za gazeti binafsi

Taarifa nchini humo zinasema mbali na ghorofa lililoanguka, nyumba nyingine zilizokua na dosari kwenye eneo hilo, zilizowekwa alama kwa ajili ya kubomolewa zilipakwa rangi upya kufuta alama zilizowekwa na mamlaka.

Matumizi ya vifaa vya ujenzi visivyo na ubora ni kawaida nchini Nigeria na serikali haichukui hatua madhubuti kuhakikisha taratibu zinafuatwa.

Wakati huohuo, ndugu wa waliokolewa wamekua wakitembelea kwa wingi hospitali tatu ambapo watu waliojeruhiwa wamefikishwa.Baadhi wamepata nafuu na kukutana na wapendwa wao wengine wakilia wasifahamu walipo watoto wao wa shule.

Mada zinazohusiana