Hasira juu ya chakula kilichooza katika jiko la wanafunzi wa Uchina

Rotten bread Haki miliki ya picha KWA HIANI
Image caption Mkate uliooza ni miongoni mwa vyakula vilivyopatikana jikoni

Moja ya shule za sekondari za kifahari nchini Uchina imekumbwa na ghadhabu ya umma baada ya rundo la vyakula vilivyooza n kupatikana kwenye jiko lake.

Mikate iliyooza na vyakula na samaki vilipatikana katika shule ya sekondari ya Chengdu No 7.

Mmoja wa wazazi aliiambia BBC juu ya hali ya kutisha na ya kutia kichefuchefu waliyoishuhudia, akisema chakula kilikuwa "kinanuka na chenye kutia kinyaa " akilinganisha jiko hilo na makazi ya nguruwe

Shule hiyo sasa imeomba radhi , ikisema ''imeaibishwa'' sana na hali hiyo.

Kashfa za chakula si jambo geni nchini Uchina namara nyingi huwaacha maafisa wakijitetea baada ya hasira ya umma.

Chakula kiligundulika vipi ?

Sakati hiyo ilitokea mara ya kwanza wakati kundi dogo la wazazi lilipokaribishwa shuleni Jumatatu kuhudhuria tukio la kupanda miti katika shule ya kibinafsi ya Chengdu, mji mkuu wa jimbo la Uchina la Sichuan.

walipokuwa shuleni, waligundua mkate mmoja uliooza, nyama na samaki wa kila aina kwenye bwalo la shule la chakula.

haijafahamika ni kwa nini waliamua kusimama upande wa jikonlakini mmoja wa wazazi aliyezungumza na BBC alielezea tukio la mwezi Novemba mwaka jana ambapo wanafunzi wengi wa shule hiyo walirudi nyumbani wakilalamika kuwa na maumivu ya tumbo, kushindwa kwenda haja na magonjwa mengine.

Haki miliki ya picha KWA HISANI
Image caption Vyakula vya baharini na nyama zilizooza viliwekwa kwenye maboxi

"[Vyakula vilionekana kama vilivyo] wekwa kwenye barafu kw amiaka mingi, ilionekana kama nyama za mizoga," alisema baba mmoja ambaye binti na kijana yake wanasomea katika shule hiyo.

"Nilihisi harufu ya nguruwe, ilikuwa inanuka . Kulikuwa na tangawizi iliyokuwa inachefua sana ."

Haki miliki ya picha Supplied
Image caption And chestnuts were seen strewn on the floor
Haki miliki ya picha KWA HISANI
Image caption Baadhi ya vyakula vilivyopatikana vimeoza

Kwa mujibu wa baba mmoja , wazazi hulipa karo ya dola $5,800 kila mwaka -ikiwa ni mara 20 ya malipo ya karo katika shule za umma .

"hatuwaruhusu watoto nyumbani waache hata chembe ya chakula ... ninatumia maelfu ya dola na wanangu wanakula mabaki ya nguruwe huko," alisema.

"Siwezi kumuambia haya kijana wangu ... nina hofu ataacha kula tena chakula cha shule. Binti yangu amekuwa akiniambia anamaumivu ya tumbo. Nilimwambia atalazimika kufanya mazoezi ya mwili

"Inanivunja moyo sana ."

Walichofanya wazazi baada ya kugundua uozo wa chakula

Wakiwa wenye kujawa na hofu, wazazi hao walisambaza picha kwenye mitandao ya kijamiiambazo baadae ziligunduliwa na wazazi wengine.

Kwa mujibu wa mzazi huyo, shule ilisafirisha mara moja chakula kilichooza kwa malori hadi mahala pengine mbali.

Lori moja lilikamatwa na kusimamishwa na umati wa wazazi wenye hasira waliokuja shuleni kuandamana kulaani yaliyoshuhudiwa, alisema.

Haki miliki ya picha KWA HISANI
Image caption mamia ya wazazi waliovamia shule kulaani chakula kilichooza

Video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii Jumatano zilionyesha mamia ya wazazi wenye ghadhabu wakiandamana nje ya lango kuu la shule.

Polisi walionekana wakitumia nguvu dhidi yao, huku video moja ikionyesha polisi wakimsukuma mwanamume mmoja ardhini.

katika video nyingine, mzazi mmoja alionekana akifikicha macho kwa maumivu, huku baadhi ya magazeti jimboni humo yakisema kuwa polisi walitumia gesi za kutoa machozi dhidi ya wazazi I

Polisi walisema wazazi walivuruga shughuli za usafiri na kuwatukana polisi. Baadae waliachiliwa

Shule ilisema nini ?

Baadae shule ya Chengdu ilitoa taarifa ya kuomba msamaha, na ikasema itaacha kuchukua chakula kutoka kwa msambazaji wao wa sasa.

Shule hiyo ni moja ya shule za kifahari zaidinchini uchina na miaka ya nyuma iliwahi kutajwa miongoni mwa shule ''10 zenye matokeo mazuri zaidi za kibinafsi nchini Uchina ".

Ilisema kuwa wahusika watashughulikiwa kikamilifu kisheria, na ikasema ''imeaibishwa'' na tukio hilo na halitawahi kutokea tena.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii