Wakenya wamepoteza matumaini katika mapambano dhidi ya rushwa?

Hands fanning out a wad of Kenyan shillings Haki miliki ya picha Getty Images

Kenya huenda imepoteza Dola milioni 210 za walipa kodi mwezi uliyopita kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Katika sakata linalofahamika kama''Sakata la mabwawa'', waendesha mashtaka wanachunguza madai kuwa pesa zilizotolewa kujenga mabwawa mawili katika eneo la bonde la ufa zimefujwa.

Wakenya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea ghadhabu zao, lakini mitandao ya kijamii haijasaidia kukabiliana na tatizo la rushwa licha ya serikali kuahidi kuwa itawachukulia hatua wahusika wa uovu huo.

Kashfa tofauti za rushwa zimewahi kufichuliwa. Washukiwa Ttofauti wamewahi kuchunguzwa kuhusiana na ufujaji wa mabilioni za fedha lakini walipa ushuru wameendelea kugharamia fedha hizo.

'Halalisheni ufisadi'

Katika sakata la hivi punde, inadaiwa kuwa kampuni moja ililipwa $80,000 kuuza vijiko, huku nyingine ikilipwa $220,000 kuuzia taasisi moja ya serikali taulo.

Hivi si vitu vya ajabu kuuzia serikali - lakini ushawahi kujiuliza: "Vitu hivi vinahusiana vipi na ujenzi wa mabwawa?"

Mmojwa wa wasanii na mwanaharakati wa kijamii nchini Kenya aliwahi kupendekeza kupitia wimbo wake kuwa ufisadi uhalalishwe nchini humo ili kila mmoja ajue ni kile kinachomkabili.

Image caption Ufisadi umekuwa tatizo kubwa Kenya

Matukio mengine ya kustaajabisha yaliyofichuliwa kuhusu ufisadi ni pamoja na kisa cha mwaka 2016, ambapo mwanamke mmoja msusi alikuwa na wakati mgumu kueleza jinsi biashara yake ilivyompatia mamilioni ya pesa kwa muda mfupi.

Msusi huyo alianzisha kampuni iliyomwezesha kupokea jumla ya $18m lutoka shirika la huduma kwa taifa - mradi wa serikali unaowafunza vijana kujitegemea.

Msusi huyo alikanusha kuhusika na sakata hiyo lakini inakadiriwa kuwa Dola milioni 78 zililipwa kwa wafanyibiahsara hewa.

Matokeo ya uchunguzi wa sakata hiyo bado hayajatolewa kwa umma.

Kashfa zilizopita za ufisadi Kenya

Haki miliki ya picha Getty Images

Sakata ya Goldenberg

Katika miaka ya 1990 wafanyikazi wa ngazi ya juu serikalini walishirikiana na kampuni ya kimataifa ya Goldenberg kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka mataifa ya yanayoendelea kwa bei nafuu.

Japo mradi lengo la mradi huo ilikuwa kuzipatia nchi hizo pesa, iliishia kuwa kashfa ya ufujaji wa mabilioni ya pesa( shilingi bilioni 60) ambyo inakadiriwa kuwa 10% ya pato jumla la serikali ya Kenya.

Maafisa wa serikali ya rais mstaafu Daniel arap baadhi yao wa ngazi ya juu walihusishwa na sakata hiyo.

Mwaka 2004 tume ya uchunguzi ilipendekeza watou kadhaa mashuhuri wachunguzwa lakini ahakuna hata mmoja aliyefungwa jela.

Sakata ya Anglo Leasing

Kashfa ya Anglo Leasing, iliyohusisha kandarasi zilizopewa mashirika ya phantom, ilifichuliwa mwaka 2004.

Fedha za kandarasi za Anglo Leasing zilikuwa takriban dola milioni 33 ambazo zililipwa na serikali ya Kenya kununua mitambo wa teknolojia ya kisasa ya kuchapisha Pasipoti; lakini kampuni zingine zilipewa kandarasi za kuleta meli na bidhaa za maabara katika hali ya kutatanisha.

Mwaka 2015, maafisa saba wa serikali walistakiwa. Kesi hiyo bado inaendelea.

Sakata ya Huduma ya vijana kwa taifa

Mwak ja na mkuu wa Shirika la huduma kwa vijana (NYS) alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya wizi wa shilingi bilioni nane.

Fedha hizo zinadaiwa kuibwa katika kashfa inayowahusishha maafisa wa ngazi ya juu serikalini ambapo wakandarasi hewa walilipwa.

Waendesha mashtaka wamewafungullia mashtaka watu 35 lakini wote wapepinga mashtaka dhidi yao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakenya wameandamana mara kadhaa kupinga ufisadi lakini hakuna tofauti kubwa iliyoshuhudiwa

Hali inazidi kuwa mbaya

Ni vigumu kukadiria wakenya wamepoteza pesa ngapi katika visa vya ulaji rushwa tangu ilipojinyakulia uhuru mwaka 1964.

Kwa mujibu wa tovuti ya trackcorruption.org inakadiriwa kuwa shilingi bilioni 66 zimepotea kupitia kashfa za ulajirushwa

Hizi ni fedha za umma ambazo zimepotea,kuibwa au kufujwa - fesha ambazo zingetumika kufanya miadi ya maendeleao kama vile kujenga shula, hopitali na mabwawa mengi ya maji.

Shirika la Transparency International hivi karibuni limetangaza kuwa hali ya ufisadi inazidi kuwa mbaya nchini Kenya.

Nchi hiyo imeorodheshwa kuwa nambari 144 kati ya 180 ya nchi fisadi zaidi duniani.

Afisa mkuu mtendaji wa Transparency International Kenya, Samuel Kimeu,mwezi Januari alisema: "Baadhi ya asasi muhimu zilizo na jukumu la kukabiliana na rushwa zinakabiliwa na changamoto kubwa kutekeleza wajimu wake kutokana na muingilio wa wanasiasa katika utendakazi wao."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiwango cha maendeleo katika kaunti mbalimbali ni tofauti

Wakili na mwanaharakati Marilyn Kamuru,alitoa wito kwa wakenya katika kipindi kimoja cha Televisheni, kuita ufisadi "wizi wa mabavu".

Watu wengi waliunga mkono tamko lake na nakuwarai wenzao kuita ufisadi jina linalostahili badala ya kutafuta majina ambayo hayana maana yoyote.

Hata hiyo maisha yanaendelea klama kawaida katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika kanda ya Afrika Mashariki.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii