China: Wazazi wavamia shule baada ya picha za vyakula vilivyooza kuvujishwa mitandaoni

Mkate uliyooza Haki miliki ya picha Supplied
Image caption Mkate uliyooza ni moja ya vyakula vilivyopatikana jikoni

Moja ya shule ya upili ya kifahari China imekosolewa vikali baada ya vyakula vilivyooza kupatikana ndani ya jiko lake.

Mikate iliyooza pamoja na nyama na samaki zilipatikana baada ya wazazi wkuvamia shule ya upili ya Chengdu.

Mmoja wa wazazi hao aliiambia BBC jinsi alivyogutushwa na harufu kali na ya ''kukirihisha'' kutoka kwa vyakula hivyo.

Shule hiyo imeomba msamaha ,ikisema kuwa imefedheheka sana na tukio hilo.

Kashfa ya usalama wa chakula sio jambo geni nchi China na mara nyingi huzifanya mamlaka kukabiliwa na wakati mgumu kukabiliana na ghadhabu kutoka kwa umma.

Vyakula hivyo vilipatikana vipi?

Kashfa hiyo iliibuka wakati kundi dogo la wazazi lilialikwa katika shughuli ya upanzi wa miti katika shule ya upili ya kibinafsi mjini Chengdu, katika mkoa wa Sichuan.

Walipokuwa hapo wazazi hao waligundua kuna mikate ya kuoza na vyakula vingine ndani ya chumba kimoja karibu na sehemu ya jiko la shule.

Haki miliki ya picha Supplied

Haijabainika kwanini waliamua kufika maeneo ya jikoni wakati shughuli ya upanzi wa miti haikuwa karibui na sehemu hiyo.

Lakini mmoja wa wazazi aliyezungumza na BBC alielezea kuwa visa vya wanafunzi kuumwa na tumbo na magonjwa mengine vimeripotiwa sana hasa mwishon wa mwaka uliyopita.

"[Vyakula hivyo vinaonekana kama vilihifadhiwa ndani ya barafu] kwa miaka kadhaa, [vinatatisha sana]," alisema mmoja wa wazazi aliye na watoto wawili katika shule.

Haki miliki ya picha Supplied
Image caption Njugu zilizokongolewa zimemwagwa sakafuni

Kwa mujibu wa mzazi huyo karo ya shule hiyo inagharimu dola 5,800 kwa mwaka kiwango ambacho ni karibu mara 20 ya karo inayotozwa shule za umma nchini China.

"Nasikitika kuwa natumia maelfu ya madola kuwasomesha wanangu katika shule hii wakati wanalishwa vyakula vilivyooza," alisema.

Taarifa hiyo imepokelewaje?

Wazazi waliyovamia jiko la shule walipiga picha vyakula hivyo na kuzisambazo katika mitandoa ya kijamii.

Haki miliki ya picha Supplied
Image caption Vyakula vivyooza

Kwa mujibu wa baadhi ya wazazi shule hiyo iliondo vyakula hivyo kwa kutumia magari mawili.

Moja ya magari hayo ilivamiwa na kuzuiliwa na wazazi waliyokuwa wakiandamana kuelekea shuleni humo.

Kanda za video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii siku ya Jumatano ziliwaonesha mamia ya wazazi waliyojawa na ghadhabu wakiaandamana nje ya lango la shule hiyo.

Haki miliki ya picha Supplied
Image caption Mamia ya wazazi waliandamana dhidi ya shule hiyo

Polisi walionekana wakitumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya wazazi hao huku baadhi yao wakikamatwa na baadaye kuachiwa huru.

Shule hiyo baadae ilitoa taarifa ya kuomba msamaha na kusema kuwa imesitisha huduma ya watu waliyokuwa wakiwaletea vyakula.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii