Ethiopian Airlines: Ibada ya maombolezo ya marehemu waliokufa katika jali ya ndege yafanyika

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jeneza likiwa na udongo uliochukuliwa kwenye eneo la ajali kwasababu haikuwezekana kupata miili ya wahanga wa ajali ya ndege

Ibada zimekuwa zikifanyika katika mataifa ya Ethiopia na Kenya kwaajili ya marehemu 157 waliokufa katika ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines iliyoanguka.

Ndegu waliangua kilio na kujitupa juu ya majeneza mekundu ya Waethiopia 12 katika kanisa kuu la Holy Trinity lililopo katika mji mkuu, Addis Ababa.

Baadhi ya majeneza yalikuwa yamewekwa udongo uliochukuliwa kwenye ardhi ya mahala ambapo ndege hiyo iliangukia kwasababu imekuwa vigumu kuipata miili ya marehemu.

Familia zimekwishaambiwa kuwa inaweza kuchukua miezi sita kuweza kubaini miili ya wapendwa wao.

Wahudumu wa Ethiopian Airlines walikusanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole International kutoa heshima zao za mwisho za wahudumu wa ndege ya Boeing 737 MAX 8 chapa 302 iliyokuwa ikieelekea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, limeripoti shirika la habari la Reuters.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wahudumu8 wa ndege ni miongoni mwa wasafiri 12 raia wa Ethiopia waliofuka katika ajali ya ndege
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption baadhi ya ndegu wa marehemu wanasema wataridhika wakati walau sehemu za miili ya wapendwa wao itakapopatikana

Mjini Nairobi, ndugu wa baadhi ya Wakenya 36 waliokufa kwenye ajali hiyo na wanadiplomasia wanaowakilisha zaidi ya nchi 30 ambazo raia wake walikufa kwenye ajali hiyo, walikusanyika katika kanisa la Orthodox la Waethiopia mjini humo.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi, ambaye amekuwa kwenye kanisa hilo, anasema kulikuwa na hali ya majonzi wakati mishumaa ilipowashwa wakati wa ibada.

Mwandishi wetu anasema awali kulikuwa na mkanganyiko jamaa waliposikia kuwa haitawezekana kuigundua miili , lakini anasema sasa imebidi wakubali hali.

Image caption Ndugu, jamaa na marafiki wa wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines wakiwa katika ibada ya wafu katika kanisa la Orthodox mjini Nairobi
Image caption Viongozi wa kanisa na Kiothodox la Ethiopia lililopo mjini Nairobi waliongoza ibada ya wafu kuwaombea wahanga wa ajali ya Ethiopian Airlines Jumapili

Baadhi ya ndugu wa marehemu wamemuambia kuwa watatulia pale walau sehemu ya miili ya wapendwa wao ilikapowasilishwa kwao.

Nchi mbali mbali kote duniani zimezuwia ndege aina ya 737 Max 8 na ndege 9 baada ya ajali ya ndege chapa 302 kuanguka tarehe 10 Machi.

Waziri wa uchukuzi wa Ethiopia amesema Jumapili kwamba inaweza kuchukua "muda mrefu " kufany auchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo iliyokuwa mpya.

"Uchunguzi wa kiwango hiki cha ajali unataka tathmini ya umakini na muda wa kutosha ilikuweza kukpata matokeo halisi," Dagmawit Mogesaliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Ndugu wa abiria waliokufa katika tukio hilo wanashauriwa kutoa sampuli zao za vinasaba DNA mjini Addis Ababa au katika ofisi za Ethiopian Airlines zilizopo katika mataifa ya kigeni.

Vyeti vya kifo vinatarajiwa kutolewa katika kipindi cha wiki bili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mishumaa iliyoyowashwa kwa ajili ya wahanga katika eneo ambapo ndege ya Ethiopian Airlines ilianguka wiki iliyopita

Familia zinazowaomboleza wapendwa wao zinapewa mfuko wa kilo moja wa udongo kuuzika kama sehemua ya ibada ya Jumapili inayofanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia , imesema ripoti ya shirika la habari la AP.

"Udongo huo umetolewa kwasababu haikuwezekana kuibaini miili na kuiwasilisha kwa familia za wahanga wa ajali ,"alisema mmoja wa ndegu wa marehemu , na kuongeza kuwa : "Hatutapumzika hadi tutakapopewa miili halisi au viungo vya wapendwa wetu ."

Waethiopia wanaochunguza sababu ya ajali hiyo wanasaidiwa na wataalam kutoka nchi mbali mbali duniani ,zikiwemo Marekani na Ufaransa.

Kisanduku cha data za safari ya ndege (FDR) pamoja na kisanduku kinachorekodi taarifa za ndege kiitwacho black box vimepatikana na wachunguzi wa ajali hiyo wanatumai vitasaidia kutoa mwangaza juu ya kilichosababisha mkasa huo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii