Mashujaa waliokabiliana na washambuliaji wa misikiti ya New Zealand watambulika

Polisi akiwa akiwa amesimama kwa ulinzi nje ya msikiti wa Al Noor siku mbili baada ya shambulio Haki miliki ya picha Getty Images

Kumekuwa na taarifa za mashujaa wakati wa shambulio la misikiti miwili iliyopo katika kanisa la Christchurch, New Zealand lililowauwa watu 50.

Mwanamume mmoja raia Afghanstan mwenye umri wa miaka 48-anasema alikabiliana na mshambuliaji aliyekuwa na silaha kwa kumrushia mashine ya malipo ya benki(credit bank machine)

Polisi wawili wa kitengo cha vijinini, mmoja wao akiwa na bunduki moja tu ya mkononi , waliweza kumkimbiza na kukamata mshqambuliaji Brenton Tarrant, mwenye umri wa miaka 28.

Mshukiwa huyo alikuwa na vilipuzi vyake ndani ya gari, na alikuwa anapangakufanya mashambulio zaidi siku hiyo , alisema Waziri Mkuu Jacinda Ardern.

Awali aliyataja mauaji hayo kama "kitendo cha ugaidi" na akasema miili ya wale waliouawa inapaswa kurejeshwa kwa jamaa zao kwa ajili ya mazishi kufikia Jumatano.

Salamu za rambirambi zimekuwa zikitolewa kwa ajili ya wahanga huku watu 34 wakiwa bado wanaendelea kupata matibabu hospitalini, akiwemo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne ambaye yuko katika hali mahututi.

Haki miliki ya picha Reuters

Abdul Aziz, aliyeondoka Kabul na kuenda New Zealand miaka kadhaa iliyopita amesema alikuwa ndani ya msikiti wa Linwood , ambao ulilengwa na mshambuliaji wa pili aliposikia kelele kwamba mtu fulani amefyatua risasi.

Wakati alipobaini kuwa wameshambuliwa, alichukua mashine ya malipo ya benki credit card na kutimua mbio kuelekea alipokuwa mshambuliaj.

Alikirusha kifaa hicho mithiri ya mashine ya kukokotoa hesabu kwenye uso wa mshambuliaji na kukimbia haraka ndani ya gari lake kuchukua silaha nyingine na kujificha katikati ya magari ndipo mshambuliaji akaanza kumfyatulia risasi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abdul Aziz anasema alimfukuza mshambuliaji mwenye silaha na kumpiga na mashine ya malipo ya benki usoni

Bwana Aziz, ambaye alikuwa ndani ya msikiti na watoto wake wanne ,alichukua bunduki iliyotupwa na mshukiwa na kuikoki , lakini ilikuwa haina risasi.

Alimfuata mshambuliaji kwa nyuma ndani ya msikiti , ambako hatimae alipambana nae tena .

" Aliponiona na bunduki fupi , aliangusha chini bunduki na kukimbia kuelekea kwenye gari lake . Nilimkimbiza ," aliliambia shirika la habari la Reuters . " Alikaa ndani ya gari lake na ... Nikatupa bunduki kupitia kwenye dirisha lake kama mshale. Aliapa tu mbele yangu na kutimua mbio."

Kaimu Imam katika msikiti wa Linwood Latef Alabi aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa idadi ya vifo ingekuwa kubwa zaidi kwenye msikiti huo kama Bwana Aziz, ambaye alisema hakumuogopa mshambuliaji asingejitolea kukabiliana na mshambuliaji.

Maofisa waliiweka New Zealand mbele kwanza ," alisema Bi Ardern Jumamosi , akiongeza kuwa watatambuliwa kwa ujasili wao, alisema Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bi Ardern.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maofisa waliiweka New Zealand mbele kwanza ," alisema Bi Ardern Jumamosi , akiongeza kuwa watatambuliwa kwa ujasili wao, alisema Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bi Ardern

Polisi wawili wa kitengo cha jamii wa vijijini waliokuwepo karibu na tukio hilo walimkimbiza mshambuliaji , wakazuwia gari lake na kumkamata.

Tukio hilo lilirekodiwa na mmoja wa watu walioshuhudia wakati huo, ambaye alituma video yake kwenye mitandao ya kijamii.

"Maofisa waliiweka New Zealand mbele," alisema Bi Ardern Jumamosi , akiongeza kuwa watatrambuliwa kwa ujasili wao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii