Ukame Kenya: Watu 11 wamefariki kutokana na uhaba wa chakula Turkana

Zaidi ya watu 800,000 wanaendelea kuumia kwa makali ya njaa na kiu kwa mujibu wa wizara ya kudhibiti majanga na utumishi wa umma ya kaunti ya Turkana.

Huyu ni mama Audan Loteng' Takwa aliye na umri wa miaka 63.
Maelezo ya picha,

Huyu ni mama Audan Loteng' Takwa aliye na umri wa miaka 63. Anaelezea masaibu anayopitia yeye na wanakijiji wenzake ambao wanahofia huenda wakaangamia kwa njaa iki serikali ya Kenya haitaingilia kati hali yao.

Maelezo ya picha,

Anna Emaret anasema amekuwa akigawana chakula na mifugo wake, lakini chakula kilipoisha, wakafa.

Maelezo ya picha,

Mama huyu ana ujauzito wa miezi sita na hajakula chochoto kwa siku tatu zilizopita.

Maelezo ya picha,

Mariam Loolio ni ajuza mwenye umri was miaka 85. Kwa siku tano anasema hajala chochote.

Maelezo ya picha,

Kwa mujibu wa mtazamo kuhusu uwepo wa chakula cha kutosha kwa Kenya 2019 , baadhi ya maeneo ya mashariki, kaskazini na kaskazini magharibi mwa Kenya ambapo kuna jamii za wafugaji, huenda zikakabiliwa na mzozo wa uhaba wa chakula.

Maelezo ya picha,

Kila mara ukame unapobisha hodi, maisha ya wakaazi na mifugo wao huwa hatarini.

Maelezo ya picha,

Mama Lakunyiko Emankor mwenye umri wa miaka 60 ni mkaazi wa kijiji cha Lotukumo katika eneo la Turkana ambalo linakabiliwa na njaa.

Maelezo ya picha,

Wakaazi wengi katika kijiji hiki hawajatia chakula chochote mdomoni kwa muda wa karibu siku 5 zilizopita.

Maelezo ya picha,

Serikali ya kaunti hiyo wiki iliyopita ilitoa hakikisho kwamba imeidhinisha mpango wa usaidizi kuwakinga wakaazi kutokana na madhara ya ukame uliopo.

Maelezo ya picha,

Kwa sasa wakaazi hawa wanalazimika kutuliza makali ya njaa kwa kula matunda ya mwituni yajulikanayo kama Mkoma.

Maelezo ya picha,

"Kuuza mifugo wakati wa mvua na kuwekeza fedha ili kujinusuru wakati wa kiangazi itasaidia pakubwa katika kuhakikisha kwamba ukame unasalia kuwa historia".

Maelezo ya picha,

Watoto pia hawajasazwa na baa hili la njaa.

Maelezo ya picha,

Huyu ni Mama Lakunyiko Emankor mwenye umri wa miaka 60 ni mkaazi wa kijiji cha Lotukumo.

Maelezo ya picha,

Huyu Mzee anapumua. Tumbo halina kitu kabisa. Alipopewa maziwa kwake ilikuwa kama muujiza.