Raisi Felix Tshisekedi achukua hatua dhidi ya Maseneta waliotuhumiwa kununua kura

DRC POLITICS Haki miliki ya picha Getty Images/AFP
Image caption Felix Tshisekedi raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, raisi Felix Tshisekedi ameamuru ufungaji wa sherehe dhidi ya maseneta wapya waliochaguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia shutuma dhidi yao kutoka kwa umma juu ya ununuzi wa kura.

Raisi Tshisekedi ameahidi kukutana na tume ya uchaguzi na maafisa wengine mwanzoni mwa wiki ijayo, inaarifiwa kuwa raisi pia alimhimiza mwendesha mashitaka wa serikali kufungua uchunguzi dhidi ya viongozi hao.

Haijafahamika dhahiri muda wa kuapishwa kwa maseneta wapya, Uchaguzi wa magavana pia umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani Basile Olongo wa DRC, alizungumza na BBC kufuatia mkutano aliohudhuria pamoja na raisi Felix Tshisekedi, wakiwemo maafisa kutoka tume ya uchaguzi nchini humo, pamoja na maofisa wengine wa serikali.

Magavana hao walitarajiwa kuchaguliwa Machi 27 na wabunge wa mkoa huo ambao wameshutumiwa kwa kuuza shahada za kupigia kura kabla ya uchaguzi .

Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Matokeo ya muda mrefu yanaonyesha kuwa rais Kabila alishinda viti vingi katika Seneti, na hivyo kuipa kambi yake nguvu ya kuongoza pande zote ikiwemo utoa kambi yake ya udhibiti wa bunge na hivyo kuwa na ushawishi mkubwa.

Wafuasi wa raisi Tshisekedi waliingia mtaani mwishoni mwa juma lililopita kushutumu tamko la uwepo wa "rushwa mbaya" katika mchakato wa kuwapata magavana na maseneta ingawa wagombea saba wa nafasi hizo walijiengua wenyewe kwenye mchakato, kabla ya kupiga kura kuwashtaki Wabunge wa mkoa kwa hadaa ya kunua shahada za wapiga kura kwa shahada moja kiasi cha dola za kimarekani elfu 50,000.

Tume ya uchaguzi nchini humo ilikataa ombi kutoka kwa mwanasheria mkuu wa erikali ya Kongo kusimamisha zoezi la upigaji kura ili kuruhusu polisi kufanya uchunguzi juu ya madai hayo.

Muungano wa wanashria wa raisi Tshisekedi i wa ushirikiano wa Tshisekedi walisema wataweka malalamiko kwa mahakama dhidi ya wabunge wao wa mkoa wanaoshukiwa kuwa wanahusika katika sakata la rushwa.

Kwa sheria, Mahakama ya Katiba nchini humo ina muda mpaka kufikia mwishoni mwa juma hili kutangaza matokeo ya wazi ya uchaguzi wama seneta.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii