Unaweza kutimua mbio za masafa kiwa na umri wa miaka 80?

Irene Obera (kushoto), Emma Maria Mazzenga na Constance Marmour walimaliza mashindano ya riadha ya dunia - World Masters Athletics Championships mwaka 2015 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Irene Obera (kushoto), Emma Maria Mazzenga na Constance Marmour walimaliza mashindano ya dunia ya riadha - Masters Athletics Championships mwaka 2015

Huku wengi wa wazee wenzao wenye umri wa miaka kati ya 80 na 90 wanakua katika hali ya kuchukulia umri wao kama muda wa kupumzika kwake mkimbiaji nyota Irene Obera mwenye umri wa miaka 85 ndio kwanza amefikia kiwango kingine cha juu.

Amevunja rekodi nyingi za dunia za mbio za marathoni za watu wenye umri wake, ni mmoja wa watu wanaokua kwa kasi katika mbio za "master athletes" wanaowakilisha watu waliofikia kiwango cha juu cha rekodi za mbio za kiwango ambacho mwili haukutarajiwa kufikia na ambacho unaweza kufanya baadae.

Mwingine ni John Starbrook, mwenye umri wa miaka 87 ambaye alikuwa mkimbiaji mkongwe zaidi aliyemaliza mbio za London Marathon za mwaka 2018.

Utafiti unaonyesha kuwa mazoezi ya mwili ni bora zaidi kuliko dawa zilizotengenezwa kwa ajili ya kuzuwia magonjwa yanayojitokeza wakati wa uzeeni kama vile maumivu ya misuli.

Kupata faida kamili, vi vema mtu akaanza mtindo huu wa mazoezi akiwa na umri wa miaka kumi na zaidi au miaka ishirini na zaidi.

Ni kipi tunachoweza kujifunza kutoka kwa wanariadha wazee?

Uchunguzi wa wakimbiaji wanaofanya vema - wenye umri wa miaka 35 na zaidi unatupatia wazo juu ya kile ambacho mwili wetu unaweza kukifanya wakati tunapoendelea kuzeeka.

Kutathmini za mida ya rekodi za dunia za wakimbiaji waliofanya vema ya kila kundi la miaka fulani bila shaka zinafichua kuwa uwezo wa mwili wa kutenda mambo huwa hauishi- kadri unavyozeeka bali huwa haushuki haraka hadi unapotimiza umri wa miaka 70.

Ni rahisi kuamini kuwa wanariadha hawa wanaishi maisha ya kuzingatia ubora wa afya zao; na pia mazowezi, wanafuata ulaji wa lishe bora na hawavuti sigara wala kunywa kiwango kikubwa.

Mazoezi yanaweza kuzuwia mchakato wa kuzeeka?

Afya bora kwa wazee wanaofanya mazoezi ya yakilinganishwa na wenzaowasiofanya mazoezi yanaweza kuwafanya watu waamini kuwa mazoezi ya mwili yanaweza kukufanya uonekana mwenye umri mdogo kuliko umri wako halisi.

Lakini ukweli ni kwamba wazee hawa wanaofanya mazowezi ya mwili wako vile wanavyotakiwa kuwa.

Miaka ya kale tulikuwa wawindaji, na miili yetu iliumwa kufanya kazi za mwili.

Hadi sasa, kama mtu mwenye umri wa miaka 80 anafanya mazoezi sawa na mtu mwenye miaka 50, ni mwenye umri mdogo anayeonekana mzee kuliko anavyopaswa kuonekana , kuliko mzee

Mara nyingi huwa tunakanganya athari za kutokuwa mchangamfu na mchakato wenyewe wa uzee na kuamini kuwa magonjwa fulani ni matokeo ya mtu kuwa mzee.

Kusema ukweli, mtindo wa maisha yetu ya kisasa unaharakisha kuzorota kwa mwili .

Hii inachangia kuzuka kwa magonjwa kama vile kisukari nambari 2 , magonjwa ya moyo na satarani.

Wengi wetu hatufanyi mazoezi vya kutosha.

Maisha yanayofaa

Si mazoezi ya mwili pekee yanayosaidia kuzuwia kuibuka kw amagonjwa mengi, yanaweza pia kutibu au kupunguza magonjwa mengine , na hivyo kuboresha maisha yetu.

tafiti za hivi karibuni za mazoezi ya kutumia baiskeli kwa watu wenye umri wa miaka kati ya 55-79 zimeonyesha kuwa wana uwezo wa kufanya kila jambo kwa haraka na kwa urahisi zaidi kwasababu karibu kila sehemu yao ya mwili iko katika hali nzuri.

Waendeshaji baiskeli pia walifanya vema katika vipimo vya uwezo wa akili na maisha bora .

Image caption Profesa Stephen Harridge (kushoto) na Profesa Norman Lazarus, mwenye umri wa miaka 82 na ana mfumo wa kinga ya mwili sawa na mtu mwenye umri wa miaka 20

Ni vema kuanza mazoezi ya mwili ukiwa na umri mdogo.

Tathmini ya watu wazima wa Marekani wenye umri kati ya miaka 50-71 ulibaini kuwa wale waliofanya mazoezi kati ya saa mbili na saa nane kwa wiki kunzia wujana wao hadi kufikia miaka sitini na zaidi walikuwa na uwezekano wa asilimia kupunguza vifo vyao kwa kati ya 29-36% l kwa sababu yoyote katika kipindi chote cha utafiti wa miaka 20.

Utafiti huo ulionyesha kuwa watu wanaoushughulisha mwili kwa mazoezi hawanabudi kuendelea na kiwango cha juu cha mazoezi ,lakini pia wale wenye umri wa miaka 40 na zaidiwana uwezo wa kufanya mazoezi ya mwili na kupata faida sawa na hizo.

Matatizo ya kisasa

Katika maisha ya ulimwengu wa sasa, kwa kiwango kikubwa tumeweza kuepuka matatizo yenye uhusiano na kutofanya mazoezi ya mwili , kwa kutegemea dawa tiba kwa usaidizi.

Lakini huku matarajio ya umri wetu wa kuishi yakiongezeka "viwango vyetu vya afya" - au kipindi chetu cha kufurahia maisha bila magonjwa hakijabadilika.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Martina Navratilova alishinda mbio katika Wimbledon mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 46

Huku watengenezaji wa dawa wakiendelea kuboresha kazi yao kila wakati, mazoezi ya mwili yanaweza kufanya vitu ambavyo dawa haziwezi kufanya.

Kwa mfano, kwa sasa hakuna dawa zinazoweza kukulinda dhidi ya kusinyaa kwa misuli ,jambo kubwa ni kupotea kwa uwezo wetu wa mwili.

Kuwa mtu unayeishi maisha ya mazoezi si bora tu kwa watu binafsi , ni muhimu pia kwa jamii nzima wakati ikiendelea kuzeeka.

Mnamo mwaka 2018, takriban Muingereza mmoja kati ya watano alikuwa na miaka zaidi ya 65, huku mmoja kati ya watu 40 akiwa na umri wa zaidi ya miaka 85.

Unaweza kufanya nini?

Si lazima watu wote wawe wanariadha wa kuwashinda wanaridha wengine kwa mbio wakiwa na umri mkubwa ; thawatakiwi kufany ahilo kuishi maisha ya afya bora.

Badala yake, fanya mazoezi madogo madogo ya mara kwa mara -kutembea au kudensi kidogo baada ya mikutano mara kwa mara ni muhimu .

Mazoezi ya mwili ni moja yapo ya jambo muhimu la kufanya iwapo unataka kuishi maisha ya afya. Hata kama hautakuwa mshindani wa riadha, kuanza mapema mazoezi katika miaka 20 na zaidi au 30 na zaidi ni jambo linaloweza kukusaidia sana baadae.

Na kama umepita wakati huo, kufanya mazoezi ya mwili ya taratibu inaweza kukusaidia kwa kiwango kizuri na kikubwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii