Kimbunga Idai: 'Hakuna aliyetarajiwa kuponea'
Huwezi kusikiliza tena

Kimbunga Idai: ‘Watu milioni 1.7 wapo katika njia kuu’ ya kimbunga Msumbiji, Zimbabwe na Malawi

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji sasa huenda ikawa ya juu na kufikia watu 1000 rais Filipe Nyusi amesema. Tayari kuna hatari ya maisha ya zaidi ya watoto 100,000 na watu wazima kufuatia kikmbunga hicho huku mito katika maeneo yaliothirika zaidi ikivunja kingo zake. Kimbunga hicho kilishuka katika mji wa bandari wa Beira siku ya Alhamisi kikiwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 177 kwa saa , lakini mashirika ya misaada yalifika katika eneo hilo siku ya Jumapili.