Kimbunga Idai: Msumbiji, Malawi na Zimbabwe zimeathiriwa

Kimbunga Idai kimesababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe katika kile ambacho Umoja wa mataifa unasema huenda ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika.

Mamilioni ya watu walikuwa kwenye njia ya moja kwa moja na kimbunga hicho huku mji wa pwani wa Beira nchini Msumbiji ukiathirika zaidi.

An image shows destruction caused by Cyclone Idai in the port city of Beira Haki miliki ya picha Reuters

Idadi ya waliyofariki nchini Msumbiji kufikia sasa ni watu 200 lakini rais Filipe Nyusi anahofia idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.

Watu 100,000 wanahitaji kuokolewa katika mji wa pwani wa Beira (hapo juu), kwa mujibu wa serikali ya Msumbiji.

A man overlooks wreckage caused by the flooding Haki miliki ya picha Getty Images

Mamia ya watu bado hawajulikani walipo huku jamaa zao wakijaribu kupekua vifusi kuwatafuta wapendwa wao.

A man searches the rubble for missing family members Haki miliki ya picha Getty Images

Nchini Zimbabwe (hapo chini), waathiriwa wanabeba jeneza la mmoja wa wanafamilia aliyefariki kuelekea katika kambi ya muda karibu na mto Ngangu.

Wooden graves are carried along a makeshift path Haki miliki ya picha Getty Images

Watu wanachimba makaburi ya kuwazika waathiriwa pamoja:

People dig multiple graves for their relatives Haki miliki ya picha Getty Images

Katika mto Umvumvu, hapo chini, wakaazi wanangalia kwa mshangao jinsi daraja la kuvuka mto huo lilivyoporomoka.

In Chimanimani, Zimbabwe, locals overlook an entire bridge that has been washed away. Haki miliki ya picha Reuters
People walk through the ravaged pavements of Beira, Mozambique Haki miliki ya picha Getty Images

Wafanyikazi wa Shirika la chakula la Umoja wa mataifa wanasema mji wa Beira (hapo juu) umeathiriwa vibaya na kimbunga hicho: "Hakuna umeme. Hakuna huduma za mawasiliano. Barabara zimeszibwa na milingoti ya umeme iliyoanguka."

A shivering woman stands outside her damaged home Haki miliki ya picha Getty Images

Baada ya majengo mengi katika yakiwa yameharibiwa na mengine kuporomoka, watu wanakabiliana na makali ya baridi na hali mbaya ya hewa.

A building home with walls taken out by the cyclone Haki miliki ya picha EMIDIO JOSINE

Nyumba zingine ziling'olewa mapaa kufuatia upepo mkali na iliyoandamana na mvua kubwa.

People gather on a destroyed section of road Haki miliki ya picha ADRIEN BARBIER

Barabara kati ya Beira na Chimoio imeharibika, hali ambayo imezifanya mashirika ya kutoa misaada kushindwa kuwafikishia waathiriwa misaada.

Children walking through mud as they are rescued Haki miliki ya picha Getty Images

Wanafunzi wa Shule ya St Charles Luanga nchini Zimbabwe, hapo juu waliokolewa na majeshi. Walijitahidi kuepuka tope lillilo funga barabara kuu wanayotumia kwenda shule

People queuing for food handouts in Zimbabwe Haki miliki ya picha Getty Images

Watu ambao mali yao yote imepotea sasa wanategemea misaada kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.

Picha iliyopigwa kutoka angani inaonesha uharibifu mkubwa uliyosababishwa na mafuriko yaliyosomba mimea shambani na nyumba na baadhi ya watu kupoteza maisha yao:

An aerial view of flooded houses in Mozambique Haki miliki ya picha EPA

Picha zote zina haki miliki.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii