Sarah:Niligundulika kuwa na Saratani nikiwa na ujauzito wa miezi saba

Sarah Hanan na mtoto wake Haki miliki ya picha Ben Hanan
Image caption Sarah Hanan alihisi maisha yake yamefika ukingoni baada ya kubainika kupata saratani

Saraha Hanan alikua kazini Daktari alipompigia simu.Alikua akiitegemea simu yake.

Siku moja kabla, ujauzito wa mtoto wake ukiwa na miezi saba, mwanamke huyu, 29 alifika hospitalini Minneapolis kwa ajili ya vipimo kama ilivyo kawaida.

''Kama majuma mawili yaliyopita hivi, nilikua nimekaa kwenye kochi na mume wangu,Ben, niligundua kitu kigumu kwenye titi langu,'' aliiambia BBC.Wapenzi hao hawakufikiria sana kuhusu hilo, waliweka katika orodha ya vipimo watakavyofanya.

''Daktari,'' Alimuita.''Ninajua inaweza kuwa si kitu, lakini unaweza kutazama ni nini hiki?''

Kabla ya kujua kinachoendelea alifanyiwa kipimo cha Ultrasound.kisha Biopsy.Na sasa simu inaita.

Habari haikua njema.

Ndani ya saa 24 ile furaha ya kupata mtoto iliondoka baada ya kupata taarifa kuwa nimekutwa na saratani,'' Sarah alikumbuka.

''Tulikua na furaha sana miezi kadhaa iliyopita.Baadae yakabadilika ghafla nikaona maisha yamekwisha.

Haki miliki ya picha Sarah Hanan
Image caption Sarah Hanan na mumewe Ben Hanan

Ben akikumbuka: ''Ilikua mzunguko kutoka kweye furaha na kuingia kwenye tiba (Chemotherapy).Iligundulika Alhamisi, Jumatatu tukamuona Daktari.

''Ilitupa hofu kidogo.Unaanza kufikiria, 'Sitaki kuwa peke yangu.Sitaki kumpoteza mke wangu na mtoto''.

''Walifanya vipimo na kugundua ni saratani inakua kwa haraka sana.

''Madaktari walituambia, kwa jinsi wanavyofahamu, tiba ya chemo haiwezi kumdhuru mtoto.Kwa kweli hatukua na namna nyingine ya kufanya.

Kwa mujibu wa taasisi ya saratani Macmillan, Chemotherapy ni tiba ambayo hutolewa iwapo wanawake ni wajawazito.

Utafiti unaonyesha kuwa watoto ambao mama zao wanafanya tiba hii ''hawaonyeshi kuwa na matatizo yeyote tofauti na watoto ambao mama zao hawako kwenye tiba hiyo'',Lakini hilo halikuweza kumtoa hofu Sarah.

''Kama mama kukaa pale, iliogopesha kuniweka hizo dawa mwilini mwangu.

''Lakini nahitaji kuwa na uwezo wa kumlea mtoto wangu.Nataka siku zote niwepo karibu naye.Hivyo nilitaka uwezekano wa kuweza kuishi uwe mkubwa kadiri inavyowezekana.

Wanawake katika hatari ya kuugua saratani wahitaji ukaguzi wa mapema

Kuku wanaotaga dawa ya saratani

Namna ya kubaini dalili na Ishara za Saratani, angalia yafuatayo

-Mabadiliko ya ngozi ya matiti

-Uvimbe kwenye kwapa karibu na titi

-Kuhisi uvimbe kwenye titi

-Maumivu ya wakati wote yasiyo ya kawaida kwenye titi au kwapani

-Kugeuka ghafla kwa ukubwa au umbo la titi

-Kutoka kwa kimiminika chochote kisicho cha kawaida kwenye matiti.

Wakati alipopata matibabu ya kwanza , uvimbe wa Sarah tayari ulikuwa umeongezeka mara dufu ukubwa wake.

Lakini pamoja na athari za tiba ya chemotherapy , ikimweo kupata mchoko na kizungu zungu , kipindi chake cha kwanza cha ujauzito kilikuwa tayari ni kibaya sana

" Ilikuwa ni karibu sawa na kipande cha keki ," alisema Sarah.

"Miezi yangu mitatu ya mwanzo ya ujauzito nilikuwa ninatapika wakati wote na nililazimika kwenda kwenye chumba cha dharura kwasababu sikuweza hata kubakiza tone la maji .

" Ukiongeza matibabu ya chemotherapy, ilikuwa ni kichefuchefu na kila nilichokula hakikuwa na ladha .

"Lakini pia nilifhamu kuwa nitapoteza nywele. Kufahamu kuwa nitakuwa mama mwenye upara lilikuwa ni jambo ambalo nilikubali, nikijua nitakuwa sawa ."

Mapema Jumatatu moja mwezi Januari , Sara alijifungua mtoto wa kiume kwa jina Noah.

"Nilitakiwa kusukuma mtoto kwa dakika zipatazo 20," alisema Sarah. "Wauguzi walikuwa wananitania kuwa sipaswi kumuelezea mama mwingine ninayopitia.

"Alitoka nje na mara moja akaanza.

"Alivuta kidole change kimoja na wakati huo mambo yote yakawa kweli. . .Tukawa wazazi pale pale ."

Haki miliki ya picha Ben Hanan
Image caption Noah alizaliwa mwezi Januari

Matibabu ya Sarah yalikuwa yamesitishwa siku tatu kabla ya kuzaliwa kwa Noah.

Yalianzishwa wiki moja tu baada ya kuzaliwa kwake.

Matibabu ya chemotherapy aliyokuwa anayapata yanamaanisha kuwa asingeliweza kumyonyesha mwanae.

"Nilikuwa natamani sana kumyonyesha mwanangu . Kuweza kumjali mwanangu kama hivyo''

"Baadhi ya wanawake huchagua kutomyonyesha mtoto wao, lakini mimi nilihisi kana kwamba nimepokonywa hilo, sikuwa na la kufanya juu ya hilo ."

Sarah hatawahi kunyonyesha kamwe.

Mwezi Machi, vipimo vya urithi vilionyesha kukatika kwa jeni za TP53 , zinazoongeza hatari ya saratani.

"Kama mama mpya ni kitu ambacho hakikuwa rahisi kukipokea ," Alisema Sarah.

"lakini ni sawa. Atakuwa tu mtoto mwenye akili, mtoto mwenye afya na atapewa tu maziwa ya kopo."

Sarah na mumewe wameweza kurejea kanisani, familia zao na marafiki kuomba msaada. Matunzo ya mtoto mchanga ni changamoto inayomkabili mzazi yoyote anayepata mtoto kwa mara ya kwanza.

Kufanya hivyo huku ukipitia matibabu ya saratani huifanya changamoto hiyo kuwa kubwa .

"Chemo inakumaliza kabisa," Alisema Sarah

"Hauwezi kujifanyia kitu chochote. Bahati nzuri tuna kanisa letu na familia zetu wanaotusaidia

"Inanivunja moyo ninaposhindwa kumsaidia Noah, lakini lazima tuwe tayari kuomba msaada."

Haki miliki ya picha Sarah Hanan
Image caption Ben,Sarah na mtoto Noah

Alisema : "Kuna uwezekano mkubwa kwamba huu ni mwanzo kabisa wa safari ndefu ya uchungu lakini ninataka watu waelewe kuwa ni kitu kinachotokea ,

" Mwanamke mmoja kati ya wanawake wajawazito 3,000 hupata saratani ya matiti. Watu wanajali sana jambo hili, lakini mara nyingi sana tunaogopa kulizungumzia."

Na kama ingekuwa sio Noah, huenda sara asingebainika kuwa ana saratani haraka, kwasababu asingekuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

''Kupata mimba kwa Sarah kuliyanusuru maisha yake. Kliniki ilisema kuwa huenda angekuwa amefariki katika kipindi cha mwaka mmoja ,"Alisema Ben.

Uvimbe wa Sarah unasinyaa, haraka kuliko kawaida .

Lakini bado safari ni ndefu.

Kama chembe chembe hai za saratani zilikuwepo wakati wa upasuaji , hatua nyingine ni kufanyiwa matibabu ya kuchoma chembe chembe hizo na baadae kufanyiwa matibabu ya homoni. Atakuwa akichukuliwa picha za skani kila mwakakwa kipindi kilichobaki cha uhai wake.

Hata hivyo amejipa moyo.

"Tunakimbia mbio za marathon. Lengo la mwaka huu ni kuwa huru na saratani''

"Hii ni sehemu ya hadithi ya Noar pia. Na siku moja nitamuambia yote kuhusu haya. Ni mtoto mchanga wa miujiza ."

Mada zinazohusiana