Kenya: Uagizaji wa samaki wa Uchina wawakosesha matumaini wavuvi

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Wavuvi wa Kenya wamekuwa wakihangaikakujikimu kimaisha

Muuzaji wa samaki Mechak Juma anapendelea kutowaambia wateja wake samaki anazouza zinatoka Uchina.

Tuko katika soko kubwa zaidi la samaki katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Ziwa Viktoria, ziwa kubwa zaidi barani Afrika.

Shughuli mbali mbali za biashara zinaendelea, lakini ni pesa kidogo sana zinazokwenda kwa wavuvi wa samaki wa eneo hilo kwa sasa.

Huku hifadhi ya samaki katika Ziwa Viktoria ikiwa imepungua sana kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita, na bei ya samaki imepanda kwa kiasi kikubwa uagizwaji wa samaki kutoka uchina kwa bei rahisi umeziba pengo la uhaba wa kitoweo hicho.

" Watu hawataki kununua samaki wa Kichina kwasababu hawaamini mchakato wa uzalishaji wa samaki, lakini hatuna la kufanya ," anasema Mechak, aliyekuwa amesimama karibu na kikapu kikubwa cha makuti kilichojaa samaki wabichi kutoka Uchina.

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Wafugaji wa samaki wa Kichina wanaweza kuwafuga kwa urahisi sana kwa kuwalisha mchele

"Watu hupenda kununua samaki wa hapa, lakini hatupati faida yoyote kwa kuwauza samaki kutoka kwa wenyeji kwa sasa ," anasema kijana mwenye umri wa miaka.

"Ni kwa kuuza samaki wa kichina ndio ninaweza kupata pesa za kutosha kuilisha familia yangu."

Samaki wanaovuliwa katika Ziwa Viktoria wamepungua kwa zaidi ya nusu kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita, kutokana na uvuvi wa kupindukia pamoja na uchafuzi wa mazingira. Katika kipindi hicho idadi ya watu imeongezeka mara dufu.

Magugumaji yaliyotanda eneo kubwa la maji, na mimea mingine iliyovamia maji, kwenye fukwe za ziwa hilo, pia imesababisha matatizo makubwa kwa wavuvi wa samaki nchini humo .

Wavuvi wa samaki katika Ziwa Viktoria nchini Kenya kwa sasa wanaagiza takribani tani 140,000 za samaki kwa mwaka, zaidi ya robo ya tani 500,000 zinazohitajika.

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Wavuvi wa Kenya wakati mwingine hawawezi kuuza samaki wote waliowavua

Makampuni ya Kichina na yale ya washirika wao nchini kenya walipata fursa, na sasa wanasemekana kuuza zaidi ya samaki wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 17 nchini kenya kwa mwaka , ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya kiwango hicho kilichouzwa miaka mitatu iliyopita.

Lilikuwa ni pengo rahisi kwa Uchina kulijaza, kwasababu samaki wa maji safi ambao wanawafuga kwa kiwango kikubwa ni aina ya Tilapia-ambao ni jamii sawa na wale wanaovuliwa katika Ziwa Viktoria. Kwa hiyo kwa mlaji wa Kenya samaki wote wanafanana na wana ladha sawa.

Samaki wa Uchina huuzwa kwa bei rahisi ikiwa ni sawa na dola 1.70 kwa kilo, ikilinganishwa na wale wanaovuliwa na wenyeji ambao huuzwa kwa 5 kwa kilo moja.

Kwa mvuvi wa Kenya Frederike Otieno, ni hali isiyo ya matumaini

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Wauzaji wa samaki nchini Kenya husita kukiri kuwa samaki wao ni wa kutoka Uchina

Muuzaji wa samaki kwa miaka 10, anasema kuwa alikuwa amezowea kupata shilingi za kenya takriban 3,000 sawa na $30; kwa siku, lakini kiwango hicho kwa sasa kimeshuka na kufikia hadi shilingi 400 za Kenya.

Mwezi Novemba mwaka jana, serikali ya Kenya iliingilia kati kujaribu kuwalinda wavuvi wa Ziwa Viktoria kwa kuweka marufuku ya uagizaji wa samaki aina ya Tilapia kutoka nje.

Lakini marufuku hiyo iliondolewa Januari baada ya balozi wa uchina nchini Kenya , Li Xuhang, kuelezea marufuku hiyo kama "vita vya biashara".

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Si samaki wote wa kichina wanaouzwa sokoni nchini Kenya wanauzwa kwa kuzingatia maagizo ya tarehe iliyowekwa

Muagizaji mkuu wa samaki wa Uchina nchini Kenya ni kampuni inayoitwa East African Sea Food. Mkurugenzi wake ni John Musafari, ambaye anasema kuwa japo samaki wanaozalishwa nchini Uchina ni wa kiwango cha juu , inawezekana kiwango chake cha chini cha bei kinatokana na kwamba samaki wanalishwa mchele ambao ni rahisi na upo kwa wingi .

Bwana Musafari anaongeza kuwa kuzalishaji wa samaki haujapiga hatua nchini Kenya kwasababu chakula cha samaki ''ni ghali sana'' nchini , kutokana na kwamba kilichopo sasa kutengenezwa na mahindi ambayo pia ndio chakula asili.

Haki miliki ya picha Jeroen van Loon
Image caption Baadhi wanasema kwamba uvuvi wa siku zijazo wa samaki katika ziwa Viktoria ni wa mashaka

Baadhi nchini Kenya wanafurahia kuongezeka kwa utegemezi wa samaki wanaoagizwa kutoka uchina, kama vile Simon anayesaidia usafirishaji wa maboksi ya samaki kote nchini kote.

"Tunashukuru kwamba kutokana na hawa Tilapia kutoka Uchina, maskini sasa wanaweza pia kupata samaki wenye virutubisho vya protini ," anasema Simon, ambaye alikana kutaja jina lake la pili .

kwa sasa anapata kiasi cha dola 300 kwa siku, kiwango ambacho kwa Wakenya wengi ni zaidi ya mshahara wao wa mwezi.

Lakini kwa Edward Oremo, afisa wa uvuvi nchini Kenya, inamaanisha ni mwisho wa biashara ya samaki katika Ziwa Viktoria.

"Kama uagizaji wa samaki wa Kichina utaendelea ...wavuvi wataendelea kukosa matumaini ya kazi yao , na Ziwa Viktoria litabaki tupu au maboti yatakuwa wazi katika kipindi cha chini ya miaka 50 ."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii