Jinsi unavyojinyima usingizi ndivyo unavyozidi kufupisha maisha yako

Wanasayansi sasa wanajua kwamba usingizi na ndoto ni muhimu katika maisha yetu na husaidia katika maswala kadhaa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanasayansi sasa wanajua kwamba usingizi na ndoto ni muhimu katika maisha yetu na husaidia katika maswala kadhaa

"Iwapo una hamu ya kutaka kuishi maisha marefu basi utalazimika kuwekeza katika kujipatia usingizi mzuri , kulingana na mtaalamu wa usingizi Matthew Walker.

Matthew, ambaye ni profesa wa sayansi ya neva na ile ya saikolojia katika chuo kikuu cha California , Berkeley ametazama data kutoka kwa mamilioni ya watu ambao wamehusika katika utafiti wa tawi la sayansi inayoangazia visa, usambazaji na udhibiti wa magonjwa na sababu nyengine zinazohusiana na afya.

"Usingizi ni kiungo muhimu cha kidemokrasia , na mfumo wa afya ambao unapatikana bure.

Na jamii ya kisayansi inaamini kwamba baada ya miaka 50 , wataalamu wa usingizi kote duniani hawatafanya tafiti za kuangazia kile ambacho kinasababishwa na usingizi, lakini je kuna kitu chochote ambacho usingizi hautupatii?

Je usingizi unatufanyia nini?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Miili yetu pamoja na ubongo hukosa kutekeleza majukumu yao vizuri

Kufikia sasa wataalam hawawezi kupata kitu chochote ambacho hakikuzwi na usingizi ama kile ambacho hukosekana wakati usingizi unapokuwa mfupi.

Sayansi imebaini kwamba ukosefu wa usingizi husababisha athari mbaya kwa miili yetu na ubongo.

Kila ugonjwa unaowauwa watu katika mataifa yalioendelea kama vile ugonjwa wa kusahau, saratani, magonjwa ya moyo, kunona kupitia kiasia, kisukari, unyogovu, wasiwasi na hata mtu kutaka kujiua unahusishwa na ukosefu a usingizi.

Mifumo yote ya kisaikilojia katika mwili wa binadamu ama hata operesheni ya akili huimarishwa wakati mtu anapolala.

Viungo hivyo vyote huathirika iwapo unakosa usingizi mwanana. Na ni sharti uwe usingizi halisi ili viungo hiyyo kuweza kuimarishwa. Dawa za kumfanya mtu apate usingizi zinahusishwa na kiwango cha juu cha hatari ya saratani, maambukizi na vifo.

Tunalala usingizi mchache ikilingnishwa na miaka 100 iliopita

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Usijizuie kulala unajidanganya mwenyewe.

Kwa hivyo usingizi ni kiungo muhimu na unapotazama data katika mataifa yalioendelea kuna tabia moja ya wazi kwamba watu wanalala muda mfupi zaidi ikilinganishwa na karne moja iliopita.

Kinachohitajika ni kwamba mtu anafaa kulala kati ya saa saba hadi nane ili kuhakikisha kuwa anakuwa na afya njema bila kusahau kwamba ni muhimu kuimarika kwa ubongo wako.

Unapolala chini ya saa saba , unaweza kuanza kuathirika kiakili na kimwili na kinga yako na utendaji wako unaanza kuathirika.

Je unawezaje kuhakikisha kuwa unajipatia usingizi mwororo usio na bughdha?

Jinsi ya kujipatia usingizi mzuri

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Upatie usingiuzi wako umuhimu mkubwa.

Kulala sio swala la kuweka kichwa chako katika mto, Eneo kubwa duniani halina giza , tunatumia wakati wetu mwingi kufyonza mwanga wa buluu kutoka kwenye skrini , kasi ya maisha ya kisasa ni kali.

Na usifikirie kupunguza usingizi unapopata wakati, unapokosa usingizi umekosa , kwa mujibu wa Profesa Walker.

Lakini unaweza kujifunza kulala zaidi na vizuri-wanasayansi wanasema kuwa unapobadili tabia utaanza kupata faida yake mara moja.

Profesa walker ambaye ameandika kitabu kwa jina Why We Sleep {Kwa nini tunalala} ana vidokezo hivi kutusaidia tulale:

1. Amka na kulala wakati mmoja kila siku.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia huyu wa China anajaribu kupata usingizi mchache katika kiti.

Kuanza kulala ni kitu rahisi: Hakikisha kwamba kila siku unaenda kulala na unaamka wakati mmoja.

Kitu muhimu ni kuweka muda utakaoamka-hilo litakusaidia kuweka muda wa kulala, kwa kuwa mwisho wa siku utahisi usingizi wakati huohuo.

Ingia katika giza

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ni lini mara ya mwisho ambapo hukuwasha taa baada ya jua kutua.

Tunahitaji kutoa homoni muhimu inayokufanya kupata usingizi mwanana

Jaribu kuweka mazingira ambayo yatasababisha usingizi kama vile kuzima taa ndani ya nyumba saa moja kabla ya kulala.

Hiyo inamaanisha kwamba zima runinga ama kompyuta kwa kuwa vifaa hivyo vina mwangaza unaoweza kuzuia homoni ya kukupatia usingizi.

Hivyobasi hufai kuona mwanga wa rangi ya buluu saa moja kabla ya kulala.

3. Tulia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Punguza viwango vya joto nyumbani kwko kabla ya kueleka kitandani.

Utulivu husababisha usingizi mwororo: Akili zetu na miili yetu inahitaji kupunguza kiwango chake cha joto hadi nyuzi joto moja ili mtu kuweza kupumzika na kupata usingizi.

Hivyobasi kumbuka kuweka nyuzi za joto hadi 18 usiku.

4. Andaa kitanda chako kwa usingizi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Utajihisi na fuaraha utakapopata usingizi mzuri.

Badaa ya kufanya vitendo vya kimapenzi , inatosha : hamufai kuwa na shindano la kula piza kushindana kusoma ama vita vya kupigana kwa kutumia mto.

Ubongo wa mwanadamu una kasi ya kufanya ushirikiano, kila mara unataka kushinikiza ujumbe.

Kitanda ni cha usingizi sio kusumbuana mukiwa na matumaini ya kupata usingizi.

Iwapo umekuwa kitandani kwa dakika 20 na hupati usingizi , ondoka na kujishirikisha na mambo mengine kama vile matembezi ama hata kusoma katika chumba kilicho na mwanga mchache hadi unapohisi uko tayari kulala.

5.Epuka vinywaji vyenye kafeini

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Usitegemee vinywaji vitakavyoweza kukukosesha usingizi ili kuendelea kufanya kazi.

Kwa siku ya kawaida tunaweza kunywa kiwango cha juu cha vinywaji vinavyoongeza utandaji wetu mwilini.

Punguza vinywaji hivyo saa 12 kabla ya kuingia kitandani , na ndio Profesa Walker anapendekeza saa 12!

Anasema kuwa kafeini zina maisha nusu: ikimaanisha kwamba saa sita baada ya kunywa bado utakuwa na kafeini nyingi katika mwili wako hivyobasi unahitaji saa 12 ili kinywaji hicho kuondoka katika mfumo wako wa neva.

6. Usinywe pombe kabla ya kuelekea kitandani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Unywaji wa pombe na baadaye ukalala sio rafiki mzuri wa usingizi

Tofauti na dhana iliopo pombe haiwezi kukusaidia kulala ama kutulia na inaweza kuhitilifaina na ndoto yako njema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii