Bangi yenye nguvu inaongeza hatari kubwa ya magonjwa ya akili, wasema watafiti

Msokoto wa bangi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wanaotumia bangi wanaweza kushindwa kuelewa mambo halisi na kushindwa kusikia sauti zao, wanasema watafiti

Kuvuta bangi yenye nguvu yenye majani 'yenye miraba myeusi na myeupe ' kunakuongezea hatari kubwa ya kupata magonjwa ya akili, wanasema watafiti.

Wanakadiria kuwa kwa wastani matukio mapya 10 yakiakili yanaweza kuhusishwa na bangi yenye nguvu, wakizingatia utafiti walioufanya kwenye miji ya ulaya.

katika miji ya London na Amsterdam, ambako nyingi kati ya bangi hizo zinauzwa ni zile zenye ukali, hatari inaweza kuwa ni ya kiwango cha juu zaidi , walisema watafiti hao katika jarida la Lancet

Haki miliki ya picha KING'S COLLEGE LONDON
Image caption ''Kama ukiamua kutumia bangi yenye nguvu ufahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuihatarisha akili yako'', wanasema watafiti

Matumizi ya bangi ya kila siku pia hufanya matatizo ya kiakili yaongezeke, walibaini.

Wataalamu wanasema watu wanapaswa kutambua hatari zinazoweza kutokea kwa afya , hata kama utafiti sio njia ya mwisho ya kuonyesha ushahidi kuwa bangi ina madhara.

Mtafiti mkuu na mtaalamu wa magonjwa ya akili Dkt Marta Di Forti anasema: "Kama ukiamua kutumia bangi yenye nguvu ufahamu kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuihatarisha akili yako ."

Dkt Adrian James kutoka Chuo cha Royal kitengo cha magonjwa ya akili alisema kuwa : "huu ni utafiti bora na matokeo yake yanafaa kupokelewa kwa umakini zaidi ."

Hatari za magonjwa ya akili

Bangi yenye nguvu husababisha watumiaji wake kupata hali ya psychosis inayomsababishia mtu kushindwa kutambua mambo, na anaweza kusikia sauti, kuona vitu ambavyo havipo au kuwa na mawazo ya mkanganyiko.

Haki miliki ya picha Getty Images

Ni hali inayotambulika kimatibabu na ni tofauti ya kuleweshwa na madawa ya kawaida.

Kuna kutoelewana juu ya kiwango gani bangi inaweza kusababisha au kuyafanya matatizo ya afya ya akili yawe mabaya zaidi na nchi nyingi zimeamua kuhalalisha kisheria au kufanya matumizi ya bangi bangi kuwa jambo ambalo si uhalifu.

madaktari wanahofu juu ya kuongezeka kwa matumizi ya bangi yenye nguvu zaidi yenye kemikali aina ya THC - inayowalewesha watumiaji.

Bangi yenye muundo wa Cheche yenye kiwango cha juu cha THC ya asilimia 14% kwa sasa ina asilimia 94% ya dawa ya kulevya inayouzwa kwenye mitaa ya London, kwa mujibu wa wataalamu.

'Bangi iliharibu maisha yangu'

Ad Gridley, ambaye kwa sasa anatumia aina tatu za dawa za matibabu ya akili, aliugua ugonjwa chizophrenia unaosababisha madhara kama vile kushindwa kutambua au kutambua mambo kinyume na uhalisi wake na alijaribu kujiua. Anaamini maradhi hayo ya akili yalisababishwa na matumizi ya bangi . Aliacha kuvuta bangi.

"Nilikuwa ninavuta sana, ilikuwa kawaida kwangu kulewa na nilianza kwa kupewa kisha nakaanza kutumia mwenyewe .

Baada ya kujaribu kujiua mara kadhaa -jambo ambalo sikulizungumzia pia - mama yangu aliniona nikiwa kwenye ghorofa nikining'iniza miguu yangu yangu, nikidensi, mara moja alijua kuna tatizo ," alikieleza kipindi cha Victoria Derbyshire.

"Katika kipindi cha saa 24 taktari alipatikana na nikapelekwa hospitalini siku iliyofuata.

Imeharibu maisha yangu kwa miaka ipatayo 10 baadae. Sikuweza kufanya lolote , na nimekuwa nikilazwa hospitalini mara kumi . Sikuwa ninafanya lolote la maana maishani mwangu.

"Nilipoacha kuvuta bangi, ugonjwa wa psychosis ukaisha. Nilikuwa natumia madawa kwa hiyo walau ubongo wangu ukaanza kuwa na kuwa na usawa.

Nilipoacha kuvuta, dalili za maradhi ya ubongo zikaanza kutoweka.

"Ningejua hatari za bangi sidhani kama ningeivuta.''

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama nchini Afrika Kusini

Utafiti

Watafiti kutoka taasisi ya King's College mjini London, waliwachunguza watumiaji wa bangi kutoka miji 11 ya Muungano wa Ulaya , ikiwemo london pamoja na mkoa mmoja wa including London, as well as Brazil.

Walilinganisha sampuli za watu 901 waliopata ugonjwa wa psychosis na watu wengine 1,237 kutoka maeneo mengine ambao hawajawahi kutumia bangi.

Walitenga aina za bangi katika viwango kwa kuwatumia washiriki kulingana na uthabiti wa afya zao , licha ya kwamba hawakufanya vipimo vyovyote vya maabaravya kupima nguvu zao moja kwa moja.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii