Tetesi za soka Ulaya Jumapili 24.03.2019: Callum,Koulibaly,Soumare,Ramsey

Callum Hudson-Odoi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester kumuwania Hudson-Odoi

Manchester United imejiunga kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji Callum Hudson-Odoi,18. (Mail)

Manchester United watapaswa kulipa pauni 130 kumchukua mlinzi wa Napoli na timu ya taifa ya Senegal Kalidou Koulibaly,27.(Mail)

Manchester United inawataka wareno kinda watatu, ambapo itawagharimu kiasi cha pauni milioni 250.Makinda hao ni mshambuliaji Joao Felix, 19, na mwenzie ambaye anacheza nafasi ya ulinzi Ruben Dias, 21 wote kutoka Benfica, pia kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes.Lakini Man U inakabiliwa na ushindani kwani watatu hao wanawaniwa pia na Man City, Juventus na Real Madrid.

Tottenham inafuatilia mshambuliaji wa Wolves Diogo Jota, 22, na kiungo wa kati wa Aston VillaJack Grealish. (Express)

Mshambuliaji wa West Brom Salomon Randon yu njiani kuelekea Newcastle majira ya joto, huku

Mkurugenzi wa masuala ya ufundi wa Ajax Marc Overmars amesema ana nia ya kuwarejesha walinzi wa Totenham Jan Vertonghen, 31, na Toby Alderweireld, 30, (Fox Sports - via Metro)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kalidou Koulibaly,27.

Everton inamfuatilia mshambuliaji wa Lille Rafael Leao, 19, wakati wakiwa na mpango wa kuwasajili washambuliaji wapya wawili majira ya joto. (Mail)

Rais wa Cagliari Tommaso Giulini amethibitisha kuwa amekuwa na majadiliano na klabu ya Chelsea na Inter Milan kuhusu kiungo wa kati Nicolo Barella, 21. (Corriere dello Sport)

Newcastle na Tottenham kwa pamoja watawania sahihi ya kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare, 20. (Star)

Arsenal imetoa kipaumbele kwa beki wa kushoto, mshambuliaji na mbadala wa Aaron Ramsey.Kocha Unao Emery anamtolea macho kiungo wa kati wa Paris St-Germain Christopher Nkunku, 21, na winga wa Renne Ismaila Sarr, 21. (Football London)

Image caption Aaron Ramsey

Bournemouth imetangaza kumuuza mlinzi Nathan Ake kwa kitita cha pauni milioni 34, huku Napoli ikimuhitaji mchezaji huyo mwenye miaka 24.(CalcioMercato)

Mlinzi wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane, 25, amewaambia wachezaji wenzie kuwa anataka kuondoka Bernabeu. (Marca - via Mirror)

Walinzi Nacho Fernandez, 29, na Jesus Vallejo, 22, ni wachezaji ambao pengine watauzwa na Real Madrid. (Marca - via Mirror)

Inter Milan wana matumaini bado ya kupata sahihi ya kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic na winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 21. (La Gazzetta dello Sport)

Mada zinazohusiana