Je, kula mayai mawili au matatu kwa siku ni hatari kiasi gani kwa afya yako?

Bacon and egg sandwich Haki miliki ya picha Getty Images

Wataalamu wamekuwa wakiumiza vichwa kwa miaka kadhaa iwapo ulaji wa mayai ni mzuri au mbaya kwa afya yako.

Yawezekana jawabu la swali hilo linategemean na mayai mangapi unakula kwa wiki - hayo ni kulingana na utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la jumuiya ya matabibu wa Marekani (JAMA).

Kwa mujibu wa jarida hilo, kula mayai mawili tu kwa siku kunaweza kusababisha magonjwa ya moyo na hata kifo cha mapema.

Hilo linatokana na kiwango kikubwa cha kolestro kinachopatikana kwenye kiini. Yai kubwa moja linakuwa na mpaka miligramu 185 za kolestro kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani - zaidi ya nusu ya kiwango cha kolestro ambacho Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri mtu ale kwa siku, miligramu 300.

Uwiano wa hatari

Utafiti wa JAMA ulichakata taarifa kutoka katika majaribio sita yaliyohusisha zaidi ya watu 30,000 katika kipindi cha miaka 17.

Watafiti wamefikia hitimisho kuwa kula miligramu zaidi ya miligramu 300 za kolestro kwa siku kunaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kwa 17% na vifo vya mapema kwa 18%.

Uwiano huo wa hatari huongezeka zaidi kwenye ulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwaulaji wa mayai, na wanasayansi wamebaini kuwa kula mayai matatu au manne kwa siku kunaongeza hatari ya magonjwa ya moyo kwa 6% na vifo vya mapema kwa 8%.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kama wewe ni mpenzi wa yai unaweza kula sehemu nyeupe na na viini vichache vya mayai

Kwa mujibu wa utafiti huo, madhara hayo ya mayai hayaathiriwi na umri, nguvu ya mwili, matumizi ya tumbaku na historia ya kuwa na shinikizo la damu.

"Utafiti wetu umebaini kuwa, endapo watu wawili watafuata aina moja ya mlo ya aina moja na tofauti pekee ikawa ni ulaji wa mayai, basi yule ambaye mwenye kula mayai mengi anauwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya moyo," anasema Norrina Allen, Profesa mshiriki wa madawa ya kinga katika Chuo Kikuu cha Northwestern University na mwandishi wa utafiti.

Tafiti za awali zitofautiana

Utafiti mpya unatofautiana na kazi za tafiti za awali ambazo zilibaini kuwa hakuna uhusiano kati ya ulaji wa yai na uwezekano wa hali ya juu wa kupata magonjwa ya moyo.

Lakini Allenanasema kwamba hazona zilikuwa na sampuli tofauti chache na zilikuwa na muda mfupi wa kufuatilia walaji wa mayai.

hata hivyo, watafiti wanakiri kuwa huenda kuna makosa katika uchunguzi wao.

Data kuhusu ulaji wa yaizilikusanywa kwa njia ya maswali ambapo ilibidi walioulizwa kukumbuka chakula chao katika kipindi cha miezi na miaka

Watafiri wengine pia walisema kuwa matokeo ni ya kuchunguzwa na ingawa walieleza uhusiano kati ya ulaji wa yai na kuongezeka kwa hatari ya ugonjwa wa moyo na kifo cha mapema, hawawezi kuthibitisha sababu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ualaji wa kiasi wa mayai unaweza kuwa muhimu katika kuepuka matatizo ya afya

"Umuhimu wa utafiti huu ni kwamba uliwakilisha ujamii tofauti za watu wa Marekani dna chakula kinacholiwa na Wamarekani wa kawaida ," anasema Tom Sanders, profesa wa masuala ya lishe katika taasisi ya King's College mjini London

"Ukomo wake unategemea kipimo cha ulaji walishe moja ."

Idadi inayoshauriwa.

Ni mayai mangapi unapaswa kula ?

Muandishi mwenza wa utafiti Allen anapendekeza usile mayai zaidi ya matatu kwa wiki.

Pia anatoa ushauri kwa wanaopenda kula mayai, mfano kula hasa sehemu nyeupe ya yai .

"Siwaambii watu wayaondoe kabisa kwenye milo yao," alisema. "Ninapendekeza tu kwamba watu wayale kiasi ."

Tom Sanders pia anasema kwamba utafiti uliuwalenga Wamarekani.

Nchi zinazoongoza duniani kwa wapenzi wa mayai kwa kuzingatia kiwango cha mayai yaliyoliwa kwa mwaka (Chanzo : International Egg Commission, 2015)
Nchi Mayai kwa kila mtu
Mexico 352
Malaysia 342
Japan 329
Urusi 285
Argentina 256
Uchina 254.8
US 252
Denmark 245

"Wastani wa kiwango cholesterol kinacholiwa na Wamarekani kinaweza kufikia karibu mayai 600, hiki kikiwa ni kiwango cha wastani wa juu kuliko kile kinacholiwa nchini Uingereza ,ambacho ni miligramu 225 kwa siku ," Tom Sanders alieleza.

Na katika takwimu za hivi karibuni kutoka Kamati ya kimataifa ya Yai , kuanzia 2015, inaonyesha kuwa Marekani ni nchi ya tano kwa ulaji zaidi wa mayai duniani - huku kila mtu akila mayai 252 kila mwaka. Lakini nchi hiyo ina matatizo ya moyo ambayo husababisha 20% ya vifo.

Japan, ambako ulaji wa mayai unafikia kiwango cha mayai 328 kwa mtu ,ilirekodi 11% pekee.

"Ulaji wa mayai jisai walau mayai 3 hadi 4 kwa wiki - ni sawa ," Waliongeza wataalamu wa Uingereza

Mada zinazohusiana