Mwalimu wa sayansi wa Kenya Peter Tabichi ameshinda tuzo ya dunia

Pater Tabichi Haki miliki ya picha Varkey Foundation
Image caption Brother Peter Tabichi amesifiwa kama "mwalimu wa kipekee" ambaye hugawa sehemu kubwa ya mshahara wake

Mwalimu wa sayansi kutoka eneo la kijijini nchini Kenya , ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi maskini zaidi , ameshinda tuzo la dola milioni moja ($1m ) kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani.

Peter Tabichi, ambaye anatoka katika shirika la kidini la Francisco , alishinda tuzo ya dunia la mwaka 2019 la mwalimu bora.

Brother Peter amesifiwa kwa mafanikio yake katika shule yenye madarasa yenye watoto wengi pamoja na vitabu vichache.

Anataka kuwaona watoto wa shule kuiona "sayansi kama njia ya kufuata " kwa ajili ya siku zao zijazo.

Tuzo hilo lilitangazwa katika sherehe iliyofanyika mjini Dubai, ambapo alitambuliwa kama mwalimu aliyejitolea kuhfanya kazi "isiyo za kawaida "kwa watoto katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la bonde la ufa nchini Kenya.

Hutoa 80% ya mshahara wake kuwasaidia watoto, katika shule ya kutwa ya sekondari ya wasichana na wavulana ya Keriko iliyopo katika kijiji cha Pwani Village, kaunti ya Nakuru, ambao vinginevyo wasingeweza kupata sare za shule na vitabu.

Kuboresha sayansi

" La muhimu si pesa," alisema Brother Peter, ambaye wanafunzi wake karibu wote wanatoka katika familia zisizojiweza. Wengi ni yatima au hawana mzazi mmoja.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 36-anataka kuwa mfano na kusaidia kuinua sayansi , si kwa Kenya tu bali kote barani Afrika.

Kuhusu ushindi wake wa tuzo, Brother Peter alielezea mafanikio ambayo vijana wa Afrika wanaweza kufikia.

"Kama mwalimu ninaefanya kazi nao nimeona matumaini ya yale ambayo wanaweza kuyafanya - udadisi wao, vipaji, uwezo wao wa kiakili na imani yao.

" Vijana wa Afrika hawatabakizwa nyuma na matarajio ya chini''. Afrika itaweza kutoa wanasayansi, wahandisi, wajasiliamali, ambao majina yao yatakuwa miongoni mwa watu maarufu katika kila kona ya dunia. Na wasichana watakuwa sehemu kubwa ya historia hii ."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wengi mingoni mwa wanafunzi husafiri zaidi ya maili nne kwenda shule, katika eneo la bonde la ufa nchini Kenya.

Katika tuzo hilo lililotolewa kutokana na shindano lililoandaliwa na Wakfu wa Varkey , Brother Peter aliwapiku washiriki wengine 10,000 waliochaguliwa kutoka nchi 179.

Ni mtawa wa shirika la Mtakatifu Francisco, la dini ya Katoliki lililoanzishwa na Mt. Francis wa Assisi katika karne ya 13.

Brother Peter anasema kuna "changamoto ya ukosefu wa vifaa " katika shule yake ukiwemo uhaba wa vitabu na waalimu .

Madarasa yenye uwezo wa kuwa na wanafunzi kati ya 35 hadi 40 hulazimika kuwa na wanafunzi 70 na 80, jambo analosema linamaanisha kuwa darasa linakuwa na wanafunzi wengi kupita kiasi, na ni tatizo kwa waalimu.

Ukosefu wa intaneti ya kuaminika unamlazimisha kusafiri hadi kwenye cyber-cafe kwa ajili ya kupakua maelezo ya masomo yake ya sayansi.

Na wengi wa wanafunzi hutembea zaidi ya maili nne kwenye barabara mbovu kufika shuleni.

Lakini Brother Peter anasema ameazimia kuwapatia fursa ya kusoma na kufikia ndoto zao.

Wanafunzi wake wamekuwa wakifanikiwa katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya sayansi, ikiwemo zawadi waliyoipata kutoka taasisi ya kemia ya Uingereza ya Royal Society of Chemistry in the UK.

Majaji walisema kuwa kazi yake katika shule "iliboresha kwa kasi kubwa mafanikio ya wanafunzi ", huku wengi sasa wakijiunga na vyuo vikuu , licha ya uhaba mkubwa wa raslimali''. za masomo.

Hali yamafunzo

Brother Peter anasema moja ya changamoto imekuwa ni kuishawishi jamii kutambua umuhimu thamani ya elimu, kutembelea familia ambazo watoto wao wamo katika hatari ya kuacha shule.

Hujaribu kubadili mitizamo ya familia ambazo zinatarajiwa mabinti zao waolewe mapema - akiwashauri kuwaacha wasichana wao waendelee na masomo.

Image caption "Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika ,"alisema mwalimu aliyeshinda tuzo, Brother Peter Tabichi

Brother Peter amesema tuzo alilopewa ni ishara ya matumaini mema.

"Ni asubuhi Afrika. Anga liko wazi. Siku bado ni changa na kuna ukurasa mtupu unaosubiri kuandikwa . Huu ni wakati wa Afrika," alisema.

Brother Peter alipongezwa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

"Peter - hadithi yako ni hadithi ya Afrika , bara changa linalolipuka kwa kipaji . Wanafunzi wako wameonyesha kuwa wanaweza kushindana miongoni mwa wanafunzi bora duniani katika sayansi, teknolojia na katika nyanja zote za jitihada za binadamu ," alisema rais wa Kenya.

Shindano hilo lililenga kuinua kiwango cha taaluma ya ualimu.

Mshindi wa tuzo hilo mwaka jana alikuwa ni mwalimu wa sanaa kutoka kaskazini mwa London Andria Zafirakou na miongoni mwa waalimu wa kwanza mwaka huu ni Andrew Moffat, mwalimu mkuu wa Birmingham ambaye amekuwa katika mzozo na walimu juu ya somo linalohusu haki ya mapenzi ya jinsia moja pamoja na watu wenaobadilisha jinsia zao- LGBT.

Muasisi wa tuzo hilo , Sunny Varkey, anasema anatumai hadithi ya Brother Peter "itawatia msukumo wale wanaotaka kuingia kwenye taaluma ya ualimu na kutoa mwangaza mkubwa wa kazi nzuri wanayoifanya waalimu kote nchini kenya na kote duniani kila siku".

"Kupokelewa kwa maelfu ya maombi na kuchaguliwa kwa washiriki wa shindano kutoka kila kona ya sayari ni ushahidi wa mafanikio ya waalimu na mafanikio makubwa waliyonayo katika maisha yetu sote ," alisema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii