Ethiopian Airlines bado wana imani na Boeing

Kifusi cha ndege ya Ethiopian Airlines nambari 302 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kifusi kilichotoka kwenye ndege ya Ethiopian Airlines nambari 02

Mkuu wa kampuni ya ndege ya Ethiopia, Ethiopian Airlines amesema kuwa bado "ana imani na Boeing" licha ya ajali iliyohusisha ndege ya aina hiyo 737 Max, iliyotengenezwa na kampuni ya Marekani ambayo iliwauwa watu 157.

Tewolde Gebremariam alisema : "Licha ya maafa , Boeing na Ethiopian Airlines wataendelea kuwa na uhusiano mwema siku zijazo ."

Kando na hayo , Bwana Tewolde pia alisema kuwa mfumo wa usalama wa ndege ulikuwa unanya kazi kabla ya mkasa.

Muundo ulibainika kuwa ndio tatizo katika ajali nyingine ya ndege ya Boeing 737 Max.

Katika taarifa iliyoainisha mahusiano baina ya makampuni ya ndege ya Ethiopia na Marekani, Bwana Tewolde alisema: "Tuwe wazi: Ethiopian Airlines inaimani na Boeing.

wamekuwa washirika wetu kwa miaka mingi ."

Pia alisema kuwa zaidi ya theluthi mbili ya safari za ndege za Ethiopia hufanywa na ndege zilizotengenezwa na Boeing.

Ethiopian Airlines pia imeagiza ndege nyingine ya zaidi ya Boeing 25 Max 737 , baada ya kununua ndege tano.

Wiki iliyopita , kampuni ya ndege ya Garuda Indonesia ilisema kuwa itafuta mpango wake wa kuagiza ndege ya za 49 Boeing 737 Max 8 aina ya jet baada ya kusema kuwa wateja wake ''wamekosa imani'' na ndege za aina hiyo.

Uagizaji wa ndege 376 kati ya 5,012 za Boeing umefutwa.

Timu ya wataalamu, wakiwemo watu kutoka wizara ya uchukuzi ya Ethiopia, wanachunguza taarifa kutoka kwenye kisanduku ukusanyaji wa sauti zandege ( black box) kilichopatikana kwenye eneo la ajali iliyotokea tarehe 10 Machi karibu na mji mkuu Addis Ababa.

Ni ajali ya pili iliyohusisha na Boeing 737 Max katika kipinchi cha chini ya miezi mitano baada ya ndege ya Lion Air kuanguka Indonesia mwezi October, na kuwauwa watu 189.

Ndege zote za Boeing 737 Max zimewekewa marufuku ya kusafiri.

'Uwazi '

Wakati huo huo, Bwana Tewolde aliliambia jarida la Wall Street kwamba mfumo wa kuzuwia ajali kwenye ndege unaojulikana kama-Maneuvering Characteristics Augmentation System (MCAS), unaonekana kuwa ulikuwa unafanya kazi kabla ajali itokee.

Ingawa alisema kuwa hajaweza kuelewa taarifa za kisanduku cha kurekodi sauti za ndani ya ndege na chumba cha rubani vilichopatikana kutoka ndege nambari 302, alisema alikuwa amesikiliza mawasiliano kati ya rubani na chumba cha kuongoza ndege kwenye uwanja wa ndege wa Addis Ababa.

Boeing inaandaa programu ya kurekebisha mfumo - ambao utatakiwa kuidhinishwa na shirika la safari za anga la Marekani -US Federal Aviation Administration - ambao umetengenezwa kwa ajili ya kuzuwia ndege kuelekeza uso wake juu katika pembe ya juu ,ambako inaweza kupoteza uwiano.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Ethiopian Airlines Tewolde GebreMariam

atika ajali ya Lion Air, iligundulika kuwa mfumo ulisukuma uso wa ndege chini mara kadhaa kabla ya ajali kutokea.

Bwana Tewolde aliliambia gazeti kwamba Boeing inapaswa kuwa na "uwazi zaidi " kuhusu mfumo wa MCAS, ambao ulikuwa mpya katika ndege ya Max aircraft ambayo ilianza safari za kibiashara mwaka 2017.

Alisema : "Na hata baada ya kuanguka kwa ndege ya Lion Air …mengi yangepaswa kuwa yamefanywa na Boeing katika kuweka wazi mchakato wa taratibu thabiti kuliko kile walichotupatia ."

Boeing ilisema kuwa itafanya "kikao cha taarifa " na marubani, waongozaji wa ndege Jumatano kujadili programu na kuwapa mafunzo juu ya utendaji wa 737 Max.

Pia kuna tetesi kwamba ripoti za awali zilizozingatia taarifa kutoka kwenye kisanduku cha kurekodi sauti za ndege ya Ethiopian Airlines (black boxes) zinaweza kutangazwa wiki hii.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii